Tatizo la mapigo ya moyo kwenda vibaya

Ingawa ‘atrial fibrillation’ haitishii maisha, kuongezeka kwa mapigo ya moyo huweza kupelekea matatizo kama vile damu kuganda ambapo hatimaye inaweza kusababisha kiharusi.
Muktasari:
Kuna nyakati waweza kujihisi kupata mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida. Je husababishwa na nini?
Mwili una mfumo asili wa umeme unaosaidia moyo kufanya kazi. Mfumo huu husababisha moyo kutanuka na kusinyaa ambapo husababisha damu kuingia na kutoka kwenye moyo. Umeme kwa kawaida hufuata mkondo na mapigo ya moyo kwa kasi ya kawaida.
Mapigo ya moyo yanapodunda kwa kiwango ambacho si cha kawaida, mfano kuwa chini au juu ya kiwango, kitaalamu inajulikana kama Cardiac Arrhythmia.
Kama mkondo wa kawaida wa umeme umevurugwa, moyo hushindwa kufanya kazi na kusababisha mapigo ya moyo ama kwenda taratibu sana, haraka sana au yasiyo imara.
Kuna aina kadhaa za Arrhythmia. Baadhi ni pamoja na zijulikanazo kitaalamu kama Supra-Ventricular Tachycardia, Ventricular Tachycardia, Ventricular Fibrillation, Atrial flutter and Atrial Fibrillation. Mapigo ya moyo yasiyo imara hasa husababishwa na ugonjwa wa moyo. Hapa moyo hushindwa kufanya kazi vizuri. Arrhythmia ndogo pia huweza kusababishwa na mtindo wa maisha usiozingatia afya bora ikiwa ni pamoja na uvutaji sigara uliopitiliza, ulevi na kuzidisha matumizi ya kafeini au msongo wa mawazo.
Ingawa imegundulika hasa katika uchunguzi wa mara kwa mara wa matibabu dalili za arrhythmia ni chache zinazoweza kuonekana ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo, kupungua kwa mapigo ya moyo, maumivu ya kifua, kizunguzungu, kuchoka sana na kukosa pumzi.
Arrhythmia mara nyingi hutokea kwa nyakati tofauti. Hali ya kutotabiri kwa arrhythmia na kutokea kwake kwa nyakati tofautitofauti hufanya uchunguzi kuwa mgumu. Moja ya vifaa vitumikavyo zaidi kwa uchunguzi wake kitaalamu ni electrophysiology (EP) na kinachukuliwa kuwa bora zaidi katika taaluma hii.
Utafiti wa EP hufanya kazi kwa kupima na kurekodi shughuli za umeme wa moyo na kuonyesha njia za umeme. Inaonyesha sababu na mahala penye tatizo la mapigo ya moyo. Matatizo yanayotokea katika utafiti wa EP ni machache sana kwa kuwa umekuwa ukifanyika salama kwa miaka mingi sasa.
Taarifa inaweza kuundwa katika namna mbili, ama kupitia ramani ya shughuli za umeme wa moyo kupitia kifaa maalumu kijulikanacho kitaalamu kama Electrocardiogram (ECG) inayoonyesha wapi ishara zisiyo za kawaida zinaanza kutokea ndani ya moyo.
Mfumo wa kitaalamu wa Carto3 ujulikanao kama 3D mapping ni teknolojia mpya inayotoa mwonekano wa moyo kwa ukubwa mara tatu zaidi. Hii huwezesha kuboreshwa kwa usahihi wa vipimo na matibabu ya mgonjwa.
Kwa kesi ya kushuka kwa mapigo ya moyo, utafiti wa EP unatoa nafasi kutathmini haja ya vifaa kama vile peacemaker au defibrillator ambavyo husaidia kuzuia vifo vya ghafla vya magonjwa ya moyo.
Baada ya uchunguzi kupitia utafiti wa EP, mirija maalumu ya Radiofrequency (RF) catheter ablation huingizwa katika mishipa ya damu ambapo viwango vya juu na vya chini vya mzunguko wa nguvu ya umeme vinavyosababisha tishu za moyo na kuharibu tishu zile zinazohusika na mapigo ya moyo arrhythmia.
Baada ya matibabu kwa kawaida wagonjwa sasa huweza kikamilifu kupunguza matumizi ya dawa ambapo mgonjwa ataweza kupumua vizuri na mapigo ya moyo kwenda vizuri.
Baadhi ya arrthythmia zilitibiwa kupitia kipimo cha RF Ablation ni Supraventrical Tachycardia (SVT), hii inatokea kwenye vyumba vya juu vya moyo na kwa ujumla inaelezewa kama moyo kupiga kwa kasi.
Zaidi Atrial Flutter (AFL) inaweza pia kutibiwa kwa upasuaji wa RF. AFL ni wakati atria inapopiga haraka sana kwa kiwango cha karibu mapigo 300 kwa dakika yanayotokea katika chumba cha juu cha moyo.
Arrhythmia nyingine maarufu inayotibiwa kwa RF ni Atrial Fibrillation (AF). Hii ni wakati uwezo wa moyo kufanya kazi zake unapunguzwa kwa mapigo yasiyo na mpangilio ya chumba cha juu cha moyo. Ingawa atrial fibrillation haitishii maisha, kuongezeka kwa mapigo ya moyo huweza kusababisha matatizo kama vile damu kuganda ambapo hatimaye inaweza kusababisha kiharusi.
Mwisho, Ventricular Tachycardia (VT) ambayo kama ikiachwa bila kutibiwa inaweza kuwa aina ya Arrhythmia ya kuhatarisha maisha. Hii hutokea wakati chumba cha chini cha moyo kikiongeza kasi ya mapigo kupita kiasi.
Baadhi ya manufaa ya kufanyiwa tiba ya upasuaji kwa mirija ni kuwa mtu atarajie mabadiliko ya haraka katika ubora wa maisha sababu ya kuongezeka kwa uwezo wake wa kufanya kazi, huduma ya matibabu iliyoboreshwa kwa jinsi mgonjwa anavyohitaji, huondoa upotevu wa muda, kupungua kwa gharama za tiba na kuokoa maisha ambapo mgonjwa anapewa nafasi nyingine ya kuishi.
Imeandaliwa na Dk A M Karthigesan, Mshauri wa tiba ya Umeme wa Moyo, Hospitali za Apollo, Chennai, India.
(maswali au maoni tuma [email protected] au 0713247889)