Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC, DC kuanza kupokea, kufuatilia matumizi ya dawa hospitalini

Muktasari:

  • Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa aahidi kuwashughulikia viongozi sekta ya afya wasiotatua changamoto za wananchi. Udhibiti matumizi, ugavi wa dawa mbioni.

Dar es Salaam. Katika kudhibiti matumizi pamoja na kuziba mianya yote ya uchepushaji dawa za hospitalini, Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa amesema kamati za ulinzi na usalama ngazi ya mkoa na wilaya zitaanza kupokea na kufuatilia matumizi ya dawa hizo.

Msingi wa hatua hiyo unatokana na uwepo wa taarifa baadhi ya watu wasio waaminifu kudhoofisha mnyororo mzima wa ugavi wa dawa hizo zinazotolewa na Bohari ya Dawa (MSD).

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi, Aprili 2, 2026 kwenye kikao kazi cha kutathimini hali ya upatikanaji wa dawa cha waziri huyo na wadau wa afya kilichofanyika makao makuu ya Bohari ya Dawa (MSD), Keko jinini Dar es Salaam.

Amesema kukiwa na udhaifu katika eneo hili ikijumuisha uwajibikaji mdogo, usimamizi hafifu ndio chanzo cha malalamiko pamoja na mianya.

Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa wakati akizungumza katika kikao kazi cha kutathimini hali ya upatikanaji wa dawa cha waziri huyo na wadau wa afya kilichofanyika Aprili 2, 2026 katika makao makuu ya Bohari ya Dawa (MSD), Keko jinini Dar es Salaam.

"Nitawasilisha hili kwa Waziri Mkuu ili kumuomba kutoa maelekezo mahususi kwa wakuu wa mikoa (RC) na wilaya (DC) pamoja na kamati zao za ulinzi na usalama kushiriki kikamilifu katika kusimamia upokeaji wa dawa na matumizi yake katika maeneo yao.

Akifafanua zaidi amesema ili kuongeza msingi wa usimamizi ni vyema Waziri Mkuu akatoa maelekezo hayo kwa wakuu kusimamia suala hilo. Dawa hazipaswi kupokewa kikawaida bali kwa umakini mkubwa.

"Dawa lazima zisimamiwe kwa umakini kuanzia uthibitisho na uwazi kwamba kilichotumwa ndicho kilichopokelewa kimehifadhiwa ipasavyo na kuingizwa kwenye mfumo wa utoaji huduma," amesema.

Mchengerwa amesema dawa lazima pia zitumike kwa matumizi yaliyokusudiwa huku akisisitiza hawatoruhusu zilizopokelewa kwa matumizi ya wananchi zichepushwe, zifichwe au zitumike nje ya utaratibu au walengwa waliokusudiwa," amesema.

Mchengerwa amesema suala la dawa ni la muhimu si kiutawala bali ni huduma na uhai, na imani kwa wananchi.

Baadhi ya wadau wa afya wakiwa katika kikao kazi cha kutathimini hali ya upatikanaji wa dawa cha Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, kilichofanyika Alhamisi, Aprili 2, 2026 katika makao makuu ya Bohari ya Dawa (MSD), Keko jinini Dar es Salaam.


Wafamasia kuwa sehemu ya menejimenti

Pia, ameagiza kwa Katibu Mkuu kwamba wafamasia kote nchini wanapaswa kuwa timu ya uongozi wa vituo husika vya kutolea huduma ya afya huku akisisitiza Sauti zao ziwe sehemu ya maamuzi.

"Kuanzia sasa wafamasia wote wawe timu ya menejimenti ya hospitali katika eneo husika. Wafamasia si watunzaji wa stoo pekee bali ni wataalamu wa msingi katika upatikanaji ushauri wa kitaalamu na usimamizi wa dawa," amesema.


Kibano wauza dawa kwa majina ya kibishara

Waziri huyo, amesema ipo changamoto ya baadhi ya watumishi kutoa maelekezo ya dawa kwa wagonjwa kwa mfumo wa jina la kibiashara la dawa husika (brand).

Amesema ni kosa kwa mgonjwa kuandikiwa jina la kibiashara la dawa kwa sababu ataambiwa dawa hiyo haipo. Hii inatokana na kuandikwa kwa jina la kibiashara ni kosa ukizingatia sheria na sera za afya.

"Uandishi wa dawa unapaswa kuzingatia jina la kitaalamu la dawa (generic) na si jina la kibiashara (brand) kwa sababu inadhoofisha imani ya wananchi na kuwakosesha huduma pamoja na usumbufu," amesisitiza.


Maduka ya dawa ndani ya vituo

Kwingineko Mchengerwa amesema maduka ya dawa ndani ya vituo vya kutolea huduma za afya yalikuwa na umuhimu wa kuboresha huduma na si kuchanganya wananchi.

"Katika baadhi y maeneo kuna changamoto ya mfumo huu kwani maduka hayo hayajaleta tofauti kwa mgonjwa kwa kuwa upatikanaji wa dawa unafuata mlolongo uleule," amesema.

Katika baadhi ya maeneo dawa zilizokiwa zinatolewa bure zimehamishiwa kwenye maduka yanayomlazimu mwananchi kununua badala ya kupata bure akisema halikubaliki.

Baadhi ya wadau wa afya wakiwa katika kikao kazi cha kutathimini hali ya upatikanaji wa dawa cha Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, kilichofanyika Alhamisi, Aprili 2, 2026 katika makao makuu ya Bohari ya Dawa (MSD), Keko jinini Dar es Salaam.


Lipeni madeni

Kuhusu madeni ya MSD, amesema madeni lazima yalipwe ili kuboresha mfumo mzima wa ugavi uendelee kuwa bora zaidi.

"Hospitali zote nchini lipeni madeni yenu. Hospitali kubwa lazima ziwe mfano wa nidhamu ya kifedha. Taasisi kubwa zikiwa na madeni ya MSD zinadhoofisha utendaji wa bohari,"

Akielezea hali ya upatikanaji wa dawa, Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daud Msasi amesema kwa sasa ni asilimia 89.3 huku akisema bado kuna malalamiko ya wananchi baadhi ya maeneo ambapo ni asilimia 10.7.

Amesema mfumo wa mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya ni himilivu na unaweza kukaa hadi miezi tisa.

Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Grace Magembe wakati akizungumza katika kikao kazi cha kutathimini hali ya upatikanaji wa dawa cha Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, kilichofanyika Alhamisi, Aprili 2, 2026 katika makao makuu ya Bohari ya Dawa (MSD), Keko jinini Dar es Salaam.


Ilichokisema MSD

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai, amesema MSD imenunua asilimia 30 ya hisa katika kiwanda cha ARV Arusha.

Amesema bohari ya dawa imeendelea kununua bidhaa za wazalishaji wa bidhaa za afya wa ndani huku lengo likiwa ni kushirikiana na wawekezaji wa ndani.

"Tunataka kupunguza ununuzi wa bidhaa kutoka kwa washitiri kwa sasa tumefikia asilimia 38 kutoka 82 na tunanunua kwa wazalishaji moja kwa moja kwa asilimia zaidi ya 60," amesema.

Amesema MSD ina changamoto ya kifedha, pia ufanisi wa ndani na madeni.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Serikali, Grace Magembe amesema lengo ni kufikia asilimia 90 ya upatikanaji wa dawa muhimu kama mwongozo wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unavyotaka.

Jambo lingine amesema upatikaji wa dawa upimwe na cheti na si mzigo uliopokelewa kutoka MSD akisema wataanza kupima kwa cheti cha dawa.

Akizungumza dawa kuisha muda wake amesema hazifiki asilimia tano kama unavyoelekeza mwongozo wa WHO akisema nchi iko chini ya asilimia moja.