Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matatizo ya usikivu na sababu zinazochangia

Christopher Peterson 

Mawimbi ya sauti huingia kwenye sikio la nje kupitia mfereji wa sikio.

Hali hii husababisha ngoma ya sikio na mifupa midogo ambayo ni milaini iliyoko ndani ya sikio inayoitwa ‘ngoma ya sikio’ iliyopo katika sikio la kati, kutetemeka. Kile kitendo cha kutetemeka kwa ngoma ya sikio, kunaruhusu mitetemo hiyo ya sauti isafiri hadi kwenye sehemu inayoitwa ‘koklia’.

Koklia inapokea mawimbi ya sauti na kusaidiana na vinyweleo vidogo vidogo visivyoweza kuonwa kwa macho ya kawaida isipokuwa kwa kutumia kifaa maalumu cha hadubini. Vinyweleo hivi vinapeleka ishara ya sauti kwenye ubongo ndipo sauti inaweza kutafsiriwa.

Iwapo ikitokea sehemu yoyote kati ya hizi ikaharibika au njia ya sauti ikaziba, inaweza kusababisha matatizo ya usikivu. Inakadiriwa zaidi ya asilimia 20 ya Watanzania wanamatatizo haya ya kutosikia vizuri na wengine hata kuwa uziwi.

Zipo zababu nyingi zinazosababisha matatizo haya. Tafiti fupi niliyoifanya, imenithibitishia kuwa watoto wanaozaliwa na matatizo haya, huchangiwa na aina ya maisha ya mama zao wanapokuwa wajawazito.

Tabia kama ya unywaji wa pombe kiasi cha kulewa, uvutaji wa sigara na baadhi ya vipodozi vikali vinavyotumiwa wakati wa ujauzito, vinamuathiri moja kwa moja mtoto aliyeko tumboni.

Hali hii hutoke wakati ujajuzito ukiwa na miezi minne wakati mtoto anapoanza kutengeneza neva za fahamu.

Lakini sambamba na hayo, matatizo haya yanaweza kuwa ya kurithi pia. Baadhi ya maradhi yanayodumu kwa muda mrefu mwilini ambayo japo hayahusiani na homa za masikio, lakini yanaweza kusababisha matatizo ya kusikia.

Baadhi ya maradhi haya yanaweza kuleta hatari kwa kukorofisha mzunguko wa damu kwenye mfumo wa sikio, hasa la ndani kuelekea kwenye ubongo. Maradhi haya ni pamoja na ya moyo, kisukari na saratani ya damu.

Baadhi ya dawa pia zinaweza kusababisha kupoteza uwezo wa kusikia.

Asilimia kubwa ya dawa tunazozitumia kila siku katika tiba ya maradhi mbali mbali, pamoja na ufanyaji wake wa kazi lakini pia zinaweza kusababisha hali nyingine tofauti mwilini ya maumivu ya kichwa, uchovu, kichefuchefu, kutapika na pia kupoteza uwezo wa kusikia. Dawa hizi hasa ni zile zinazotumika kutuliza maumivu na zile zinazotumika kwenye tiba za saratani.

Hata hivyo, matatizo yanayotokana na matumizi ya dawa huwa ni ya muda tu, na baadaye mwili unakuwa sawa utakapomaliza kutumia dawa hizo.

Maradhi ya utotoni nayo yanasababisha kupoteza uwezo wa kusikia. Maambukizi ya sikio yanaweza kusababisha kujaa kwa utando mzito kwenye sikio la ndani na kusababisha matatizo ya usikiaji ambayo yanaisha baada ya utando huo kuondolewa.

Maambukizi mengine yanaweza kusababisha uharifu wa sikio la kati na hata la ndani na kumfanya mtoto kuwa kiziwi.

Maradhi yanayoshambulia sana mfumo wa usikiaji kwa watoto ni pamoja na ‘chickenpox’, surua, degedege na malaria sugu kwa watoto.

Wazazi wanashauriwa pia kuwapitia watoto vyakula vyenye lishe kwa wingi ili kuwakinga na maradhi nyemelezi yatakayoathiri mifumo ya fahamu katika ukuaji wao.

Umri pia unachangia kupoteza uwezo wa kusikia. Kadri umri unavyokwenda, ndipo uwezo wa kusikia unapungua.

Hii inatokea hata kama umekuwa ukiyalinda masikio yako wakati wote. Kwa kawaida matatizo ya kupoteza uwezo wa kusikia yanayotokana na umri, huwezi kuyazuia. Watu wenye miaka 65 na kuendelea wapo hatarini kuanza kupoteza uwezo wa kusikia.