Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe ukwaju hutibu tatizo la nyongo, soma hapa

Muktasari:

  • Unachopaswa kujua leo ni kwamba, moja kati ya sifa kubwa ya ukwaju mwilini ni kutibu matatizo ya nyongo, huondoa tatizo la mtu kuvimba lakini husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo).

Ukwaju ni tunda lenye faida nyingi na matumizi mbalimbali katika mwili kuanzia kiafya, ngozi na urembo.

Unachopaswa kujua leo ni kwamba, moja kati ya sifa kubwa ya ukwaju mwilini ni kutibu matatizo ya nyongo, huondoa tatizo la mtu kuvimba lakini husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo).

Unywaji wa juisi ya ukwaju iliyochangaywa na pilipili manga, hiliki na mdalasini husaidia mtu kupata hamu ya kula pamaoja na kupata ladha ya chakula mdomoni.

Ukwaju ni chanzo cha vitamin B na C, lakini pia husaidia kuongeza nguvu na uchangamfu wa mwili, hutibu kuwashwa kwa koo na homa ya manjano.

Ukwaju pia husaidia myeyusho na mmeng’enyo wa chakula tumboni, husaidia kurahisisha uapataji wa choo, hushusha joto la mwili na huondoa homa.

Wataalamu wa afya wanashauri unywaji wa glasi moja ya juisi ya ukwaju kwa siku, huleta matokeo mazuri kwa afya ya mwili.

Pia, huulinda mwili dhidi ya mafua, hupunguza wingi wa lehemu na kuimarisha afya ya moyo.

Katika ngozi; ukwaju husaidia kung’arisha ngozi, husaidia ngozi kuwa nyororo, huondoa weusi kwenye shingo na kutibu chunusi kwa kupaka sehemu hizo.

Upande wa urembo, ukwaju husaidia kuzuia kukatika kwa nywele, husaidia kutibu ngozi yenye mafuta huku ikisaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au ngozi yenye vidonda kwa kupaka juisi ya ukwaju katika sehemu hizo na kuacha ikauke kwa muda wa dakika 20 kisha unaosha na maji ya uvuguvugu.