Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zitto ataka sera, sheria mpya mashirika ya umma

Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe akiwasilisha mada katika mkutano wa watendaji wa Taasisi na Mashirika ya Umma. Picha na Mussa Juma.

Muktasari:

  • Zitto pia ameshauri Serikali kuunda shirika moja la kusimamia hisa za serikali katika Kampuni binafsi ambazo zinazowekezwa nchini.

Arusha. Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuna haja ya kutungwa upya kwa Sera na sheria ya mashirika ya umma ili kuboresha utendaji wa mashirika ya umma.

Akitoa mada leo Agosti 19, katika mkutano wa watendaji wa taasisi na mashirika ya umma unaoendelea jijini Arusha, Zitto amesema sheria mpya ya mashirika ya umma itaweka mwongozo wa upatikanaji wakurugenzi wa bodi, watendaji wa bodi, hisa na uendeshaji.

Zitto alisema hivi sasa Kila Kampuni inayokuja hasa katika madini serikali inalazimika kuunda Kampuni ya kusimamia hisa zake chache hivyo kutakuwa na Kampuni nyingi sana.

"Lakini pia Kampuni ikiundwa tuipeleke kwenye soko la hisa ambapo Watanzania wengi watanunua hisa," amesema.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu ametaka uwepo wa maboresho ya Utendaji katika uendeshaji wa Mashirika ya umma nchini ili kwendana na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan

Mchechu amesema, ofisi yake imeandaa mkutano huo ambao utakuwa ukifanyika kila mwaka ili kuboresha utendaji wa taasisi za umma lakini pia kuja na mabadilikoambayo yataongeza ufanisi na kufikia malengo ya serikali.

"Kikao hiki ni nafasi za kuzungumza changamoto zetu na kujadiliana jinsi ya kuzitatua kwa pamoja kwani taasisi zetu zinamahusiano ya karibu,"amesema

Mkutano huo wa siku tatu unaendeleaje katika kituo cha mikutano cha Arusha (AICC) ukiwakitanisha Mawaziri, makatibu wakuu wa wizara, watendaji wa Serikali na wajumbe wa bodi za mashirika ya umma na taasisi zake.