Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau washauri mabadiliko kimuundo mashirka ya umma

Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad akizungumza katika mkutano wa watendaji wa mashirika na Taasisi za umma.

Muktasari:

  • Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, amependekeza namna bora ya upatikanaji wa wajumbe, bodi za mashirika ya umma nchini, akitaka waombe na wafanyiwe usaili.

Arusha. Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, amependekeza namna bora ya upatikanaji wa wajumbe, bodi za mashirika ya umma nchini, akitaka waombe na wafanyiwe usaili.

 Akitoa mada katika undeshaji wa mashirika hayo, na tafakuri kuhusu Tanzania, leo Agosti 19, 2023 jijini Arusha, katika mkutano wa watendaji wa mashirika ya umma nchini, Profesa Assad upatikanaji wa wajumbe wa bodi ni tatizo.

Profesa Assad amesema ili bodi za mashirika hayo ziweze kufanya kazi kwa ufanisi, lazima wajumbe wanaopatikana wawe na uwezo wa kusaidia taasisi hizo.

Amesema pia matatizo mengine yaliyosababisha mengi ya mashirika hayo ama kufa, au kufanya kazi chini ni kiwango, ni matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za taasisi, ikiwemo ununuzi wa magari ya kifahari.

"Kuna haja gani kuwanunuliwa watendaji watano katika taasisi moja, magari matano ya kisasa V8 ambapo inabidi kuajiri madereva, lazima maeneo ya kuegesha magari," amesema

Amesema sio kila wakati maafisa hao wote watakuwa safarini wakitumia magari hivyo inapaswa kuwa na magari machache hata matatu na watendaji wakatumia kwa zamu.

"Lakini pia kuna hili nimeona, tunakuja Arusha kwenye mkutano, watendaji wanakuja na ndege na magari yanawafuata Arusha, ili waje kutembelea nadhani hii pia ni matumizi mabaya ya rasilimali za mashirika," amesema.

Amesema pia kuna tatizo la bodi na watendaji wa mashirika kuingiliwa na viongozi juu wa Serikali na hivyo kutolewa maamuzi ambayo yanaathiri mashirika.

"Kwa mfano tunanunua ndege Dreamliner ambazo tunajua kabisa matumizi yake hatuwezi kwani ndege ambazo zinahitajika sana ni za kufanya safari za ndani matokeo yake shirika kupata hasara," amesema.

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, pia hakuwa mbali na Profesa Assad, kwani wakati akitoa mada yake, alipendekeza watendaji wa mashirika ya umma kuajiriwa na bodi.

"Mapendekezo yangu mimi ni kuwa Rais akiteua Mwenyekiti wa Bodi, basi bodi ndio ipewe jukumu la kuajiri Mtendaji Mkuu wa Shirika ili aweze kuwajibika kwa bodi," amesema.

Zitto amesema kumekuwepo na mgongano baina ya bodi na watendaji hao kwani kila mmoja ameteuliwa na Rais.

"Bodi ikiajiri Mtendaji Mkuu, inauwezo wa kumuondoa kama atashindwa kutekeleza majukumu yake na kuajiri mtendaji mwingin," amesema.