Zimamoto waudhibiti moto katika jengo lenye ofisi za TRA Dar

Dar es Salaam. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dar es Salaam limefanikiwa kuudhibiti moto uliozuka katika jengo lenye ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kariakoo.
Mashuhuda wamedai kuwa moto huo ulianza saa 6 mchana leo Alhamisi Januari 30, 2025 na umeathiri ‘floor’ moja ya jengo hili lililo karibu na jengo la ushirika.

Hata hivyo, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limefanikiwa kuudhibiti moto huo usiendelee kuathiri maeneo mengine huku Kamishna wa TRA, Yusuph Mwenda akiwa miongoni mwa waliofika eneo la tukio kufuatilia kwa karibu shughuli hiyo inavyofanyika.

Endelea kufuatilia Mwananchi Digital kwa taarifa zaidi