Zimamoto waandika historia Karagwe

Muktasari:
Kutokana na Serikali kukabidhi gari la kuzimia moto, wadau wamechanga zaidi ya Sh23.2 milioni kwa ajili ya ununuzi wa tangi la maji na miundombinu mingine ya gari hilo.
Karagwe. Tangu dunia hii kuumbwa, ilikuwa haijawahi Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kumiliki gari lake la zimamoto, huku huduma zote za uokoaji zilikuwa zikitegemewa kutoka Bukoba Mjini ambako kuna umbali wa kilomita 120.
Kutokana na Serikali kukabidhi gari la kuzimia moto, wadau wamechanga zaidi ya Sh23.2 milioni kwa ajili ya ununuzi wa tangi la maji na miundombinu mingine ya gari hilo.
Fedha hizo zilichangwa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Salimu Kijuu kukabidhi gari hilo ili kukabiliana na majanga ya moto.
Ofisa wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wilaya za Karagwe na Kyerwa, Peter Mbare alisema ofisi zao zilianzishwa mwaka 2014 wakiwa na askari wawili na sasa wapo watano ilhali mahitaji ni 25.
Kwa taarifa zaidi nunua gazeti lako la Mwananchi au soma mtandaoni kupitia www.epaper.mcl.co.tz