Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zambia yafunga mipaka, wafanyabiashara wa Kitanzania hoi

Muktasari:

  • Inadaiwa kwamba Serikali ya Zambia mwaka jana ilinunua shehena ya mahindi Kwa wakulima baada ya nchi hiyo kuwa na uhitaji mkubwa hali iliyoilazimu kununua kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya wananchi wake.

Songwe. Watanzania wanaofanya biashara ya mazo ya nafaka, wamejikuta katika wakati mgumu baada ya Mamlaka nchini Zambia kuzuia shehena zao na hivyo kuzusha hofu ya kupoza mitaji yao kufuatia serikali hiyo kufung mipaka kama njia ya kujihami na baa la njaa.

Inadaiwa kwamba Serikali ya Zambia mwaka jana ilinunua shehena ya mahindi kwa wakulima baada ya nchi hiyo kuwa na uhitaji mkubwa hali iliyoilazimu kununua kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya wananchi wake.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tunduma, Frank Mwakajoka kwenye mkutano wa hadhara ambapo alisema wafanyabiashara wa Tunduma hawana soko la uhakika kuuza mahindi yao baada ya nchi ya Zambia kuwa na mahindi ya kutosha.

Kutokana na hali hiyo aliiomba Serikali kuingilia kati suala hilo ikiwa ni pamoja na kuwatafutia soko la uhakika wafanyabiashara ili mipaka ya kibiashara iendelee kufunguliwa.

“Wafanyabiashara wa Tanzania walianza kununua mahindi Juni 2022 nchini Zambia na kuyauza katika eneo maarufu la biashara la Nakonde lakini cha ajabu ilipofika Novemba 2022 Serikali ya Zambia ilianza kugoma kuwapatia mahindi waliolipia wafanyabiashara hao wa Tanzania jambo hili limeleta mkanganyiko,”alisema Mwakajoka.

Alisema walipeleka malalamiko yao kwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia ndipo wachache wakapewa lakini hata waliopewa baada ya kupakia mahindi hayo yakazuiliwa njiani katika maeneo ya Kapirimposhi, Mpika, Lusaka na Kasama kabla ya kuyashusha sokoni Nakonde.

Kufuatia hali ya sintofahamu kuhusu hatina ya mahindi ya wafanyabiashara hao mkuu wa mkoa Songwe Dkt Francis Michael amekutana na wafanyabiashara hao mjini Tunduma leo na kuzungumza nao ambapo aliwataka kuwa watulivu wakati Serikali inaendelea kufanya mazungumzo na Serikali ya Zambia.