Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakulima Tanzania kupatiwa ghala Kenya

Nairobi. Wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya chakula mbalimbali ikiwemo mahindi  na kahawa wamepatiwa ghala kwa ajili ya kuhifadhia mazao yao ambayo wanayapeleka Nairobi nchini Kenya kwaajili ya kuuza, Ili kuwaondolea adha ya kuuza kwa madalali.


Wakizungumza na Mwananchi wakati wa kikao kati ya wakulima kutoka Tanzania ambao wameenda kwenye maonyesho ya AGRI-AFRICA kwa Mwaliko wa TCCIA -Turkey  ambao uliandaliwa na Dk Hamis Simba na wafanyabiashara wa  Kenya kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania Jijijini Nairobi, Kiongozi wa wafanyabiashara wa mazao ya nafaka, Eddy Mburu katika soko la Markiti alisema wameshaweka utaratibu mzuri kwa wakulima wanaotoka Tanzania kwa ajili ya kupeleka mazao yao nchini humo.

"Tuna uhaba mkubwa wa nafaka hasa mahindi hivyo tunategemea kupata mahindi na mchele kutoka Tanzania, pia tunahitaji kahawa, matunda, njegere na vitunguu toka kwenu, karibuni sana kuleta bidhaa zenu hapa, tumeandaa utaratibu na ni vyema muonane na uongozi wa soko pindi mtakapoleta bidhaa ili tuwaonyeshe sehemu ya kuhifadhia," alisema Mburu


Naye Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dk John Simbachawene amewataka wakulima ambao wanataka kuuza mazao yao nchini humo kupitia ubalozi ili mali zao ziwe salama badala ya kuuza kienyeji na inapotokea shida ndio wanakimbilia ubalozini.


"Nimefarijika wakulima  mmeziona fursa zilizopo Nairobi ni nyingi hasa upande wa chakula kuna uhitaji mkubwa mno, mmetambua na kuthamini Ubalozi wenu na mmefika, hapa ndio salama kwenu niwaombe mtumie sana ubalozi huu ili kila kitu kwenye biashara zenu ziwe salama, nawahakikishia  mimi na maofisa wangu  tutawapatia ushirikiano mkubwa," alisema Dk Simbachamwene

Alisema tayari amewaagiza Bodi ya Mazao mchanganyiko kuhakikisha inafunguliwa kituo cha kuhifadhia mazao ya wakulima wanapata ghala hilo ili waweze kuhifadhia mazao na kuondokana na adha waliyokuwa wanapata awali.

Naye mkulima wa mahindi na kahawa kutoka Karagwe mkoani Kagera,  Xavier France Ntakwendera alisema kupitia maonyesho ya AGRI-AFRICA amefurahi kukutana na wakulima na wafanyabiashara wakubwa kutoka mataifa mbalimbali  ambao wamekubali kuingia makubaliano na chama chake cha Msingi cha  Nguvumali AMCOS Karagwe kununua mahindi, maharage na kahawa na wamempatia mbalimbali za kuzalisha zaidi .

Naye Mkulima Salima Mapunda kutoka Songea amesema wamejifunza mambo mengi Kenya hivyo wanaenda kujipanga na kuanza rasmi kufanya biashara ya kupeleka nafaka Kenya kwani fursa hiyo imefika wakati mwafaka wakulima wanamazao mengi na tayari wameshaanza kuvuna.

Kwa upande wake Mkuu wa msafara huo, Adam Ngamange ameishukuru ubalozi wa Tanzania nchini humo kwa kusimamia na kutafuta masoko ya wakulima kwani jitihada hizo zitazaa matunda ya falsafa ya Rais Samia Hassan kuwa  balozi ziwe fursa ya kuuza uchumi kwa Watanzania kimataifa.