Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yasiyofahamika kwa wengi kuhusu daraja la JPM a.k.a Kigongo-Busisi

Muonekano wa picha ya juu la daraja la JPM maarufu kama daraja la Kigongo-Busisi linalounganisha Wilaya za Misungwi na Sengerema mkoani Mwanza. Daraja hilo linalojengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh716 bilioni linapita juu ya maji ya Ziwa Victoria.

Muktasari:

Kwa Bara la Afrika, daraja la JPM ni la sita kwa urefu nyuma ya daraja refu kuliko zote barani Afrika lililopo nchini Misri linaloongoza kwa kuwa na urefu wa kilomita 20.5, ikifuatiwa na daraja lingine lililoko nchini Nigeria lenye urefu wa kilomita 11. Madaraja mengine marefu ni Sue canal lenye urefu wa kilomita 3.9 na zingine mbili zilizoko nchini Msumbiji zenye urefu wa kilomita 3.8 na 3.6.

Mwanza. Kwa wengi, urahisi wa kuvuka kutoka eneo la Kigongo, Wilaya ya Misungwi kwenda Busisi Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza ndio faida kuu ya ujenzi wa daraja la JPM maarufu kama Kigongo-Busisi; lakini kiuhalisia, zipo faida kadhaa zilizojificha.

Kupungua kwa muda wa kati ya dakika 45 hadi saa moja kuvuka eneo la Kigongo-Busisi kwa kutumia vivuko vya MV Mwanza na MV Misungwi hadi kufikia dakika 5 kwa kutumia gari na dakika 15 kwa waenda kwa miguu ni moja ya faida kuu za utekelezaji wa mradi huu.

Katika orodha ya faida za mradi huo, maendeleo ya kiuchumi, kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma za rufaa na wataalam wazawa kupata ujuzi, maarifa teknolojia mpya ya ujenzi wa miundombinu ya barabara ni faida nyingine inayotokana na mradi huo.

Mradi huo unaotekelezwa na mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation na China Railway 15 Bureau Group Corporation kwa kwa gharama ya Sh716.33 bilioni ulianza Februari 25, 2020 na unatarajiwa kukamilika Februari 24, 2024.

Zaidi ya Sh699.3 bilioni za mradi huo ni gharama za mkandarasi wakati mwandisi mshauri nalipwa Sh11.1 biloni, Sh3.14 zimetumika kuwalipa fidia wananchi kupisha mradi huku Sh2.8 zilitumika kufanya usanifu wa mradi.

Akizungumza na waandishi wa habari wanaotembelea miradi ya miundombinu ya barabara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) Mkoa wa Mwanza, Paschal Ambrose amesema ujenzi wa daraja hilo lenye urefu kilomita 3 na upana wa mita 28.45 umefikia zaidi ya asilimia 78.06.

‘’Kuanzia Machi, 2023, mkandarasi anafanya kazi kwa Saa 24 kufidia muda uliopotea kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Uviko-19; lengo ni kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa muda uliopangwa,’’ anasema meneja huyo

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Mohamed Besta wakati wa ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyetembelea mradi huo Juni 14, 202, changamoto zilizoshuhudiwa mwanzoni mwa utekelezaji wa mradi huo ni kuongezeka kwa kina cha maji Ziwa Victoria na tofauti ya hali ya kijiolojia.

Upekee wa daraja la JPM

Itakapokamilika, daraja hilo litakalokuwa refu kuliko yote katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati litakuwa na njia mbili za magari zenye upana wa mita saba kila upande, njia ya waenda kwa miguu yenye upana wa mita 2.5 kila upande, maegesho ya dharura yenye upana wa mita 2.5 kila upande na njia ya waenda kwa miguu yenye upana wa mita 2.5.

Daraja hilo linalopita juu ya maji ya Ziwa Victoria kuunganisha eneo la Kigongo Wilaya ya Misungwi na Busisi Wilaya ya Sengerema litakuwa na urefu wa kilomita 3, upana wa mita 28.45 na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 1.66 litakuwa daraja la sita kwa urefu katika Bara la Afrika.

Nguzo za 804, kitako cha nguzo za madaraja 65, nguzo kuu 67 zikiwemo nguzo kuu tatu na nguzo za mlalo 806 ni miongoni mwa mambo ya kipekee katika mradi wa ujenzi wa daraja la JPM lililopewa jina hilo kama sehemu ya kutambua, kuenzi na kumbukumbu ya Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli aliyeasisi wazo na kuanza utekelezaji wa mradi huo.

Daraja la JPM pia lina upenyo mita 120 kati ya nguzo zake kuu kuruhusu meli na vyombo vingine vya usafirishaji majini kupita na hivyo kuwa daraja lenye upenye mkubwa zaidi nchini kulinganisha na daraja la Tanzanite na Kigamboni za jijini Dar es Salaam zenye upenye wa mita 100 na 120 kati ya nguzo zake kuu.

Faida za kiuchumi

William Sanga, Msimamizi wa mradi huo kutoka Tanroads anasema kukamilika kwa ujenzi wa daraja la JPM kuna faida kadhaa ikiwemo ongezeko la shughuli za kiuchumi ndani na nje ya mikoa ya Kanda ya Ziwa, Tanzania kwa ujumla na nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Anasema Kijiografia, daraja la JPM limejengwa katika eneo la ushoroba wa Ziwa Victoria kuanzia mpaka wa Sirari Wilaya ya Tarime mpakani na nchi ya Kenya hadi mpaka wa Mtukula Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera inayopakana na nchi ya Uganda; na mpaka wa Rusumo na Kabanga Wilaya ya Ngara inayopakana na nchi jirani za Rwanda na Burundi.

‘’Hii itachochea biashara na shughuli zingine za kiuchumi na hivyo kuongeza siyo tu pato la wananchi, bali pia Serikali,’’ anasema Sanga

Halima Mohamed, mkazi wa Geita anasema kukamilika kwa mradi huo utaokoa maisha ya wagonjwa kutoka mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma ambao baadhi yao maisha yao yanahatarishwa kwa kusubiri kivuko kwa muda mrefu wanapopewa rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando jijini Mwanza.

‘’Nimewahi kusubiri zaidi ya saa nzima kuvuka kutoka Busisi kwenda Kigongo kumuwahisha mtoto wangu mgonjwa Hospitali ya Bugando; hali ya mtoto ilibadilika tukiwa eneo la kivuko na nilipofika hospitali nilipelekwa moja kwa moja ICU (chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum). Daraja hili litatuokoa na adha hiyo,’’ anasema Halima

Ujuzi, maarifa na teknolojia mpya

Mhandisi Mshauri mradi wa daraja la JPM, Abdulkarim Majuto anataja ujuzi, maarifa na teknolojia mpya kwa wahandisi na mafundi wazawa wanaoshiriki utekelezaji wa mradi huo kuwa faida nyingine kwa Taifa.

“Teknolojia za kisasa na usanifu zinazotumika katika mradi wa ujenzi wa daraja hili ni fursa kwa wahandisi, mafundi na waajiriwa wa ndani kujifunza kwa kupata ujuzi kutoka kwa wenzao wa nje, ni dhahiri ujuzi huo utatumika kutekeleza miradi mingine ya aina hii siku zijazo,” anasema Abdulkarim

Utekelezaji wa mradi huo unahusisha makandarasi 17 wa ndani, watoa huduma 20 na zaidi ya wahandisi 1,200 na wafanyakazi kadhaa wenye ujuzi wa Kitanzania wenye ajira za kudumu na za muda.

Ujenzi wa daraja hilo pia unatumika kama darasa kwa wataalamu wa ndani ambapo wahandisi wanne kutoka Tanroads wanafanya kazi hapo muda wote kwa ajili ya kujifunza.

Wahandisi wahitimu 11 walioko chini ya mpango unaoratibiwa na Bodi ya Usajili Wahandisi nchini (ERB) nao wanashiriki utekelezaji wa mradi huo kwa lengo la kuwapa ujuzi na maarifa ya teknolojia mpya na ya kisasa utakaotumika katika miradi mbalimbali itakayotekelezwa nchini.