Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wizara yaridhishwa utekelezaji mradi wa maji Kiwira

Chanzo cha maji Mto Kiwira kinachotaraji  kuzalisha maji lita 117 million na kuwa mwarobaini wa maji mkoani Mbeya na Songwe. Picha na Hawa Mathias.

Muktasari:

  • Wizara yaridhishwa utekelezaji mradi wa maji utakaozalisha lita milioni 117 kwa siku

Rungwe. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi, Nadhifa Kemikimba ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa Maji kutoka chanzo cha mto Kiwira utakaozalisha lita 117 milioni kwa siku.

 Mradi huo umeelezwa kukamilika ifikapo Septemba 2025 na utaondoa changamoto ya maji katika Mkoa wa Mbeya na Songwe.

Mhandisi, Kemikimba amesema leo Jumatatu Julai 31 baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukagua miradi ya maji katika Wilaya ya Rungwe ba Chunya Mkoa wa Mbeya hususani chanzo cha maji mto Kiwira na bwawa na Matwiga.

“Niwapongeza kwa kasi ya mradi huu ambao utakuwa mwarobaini wa kumaliza tatizo la maji na ndiyo malengo makubwa ya chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kumtua Mama ndoo kichwani,” amesema.

Aidha katika ziara yake amekagua ujenzi wa bwawa la Maji Matwiga Wilaya ya Chunya ambalo litazalisha maji lita 93 milioni na kuhudumua vijiji vya pembezoni mwa Kata za Binti manyanga, Makongorosi na Matwiga.

”Nimeridhishwa na utekelezaji wa miradi licha ya kuwepo kwa changamoto ndogondogo hususan kwenye miradi ya visima hivyo nimewapa muda wa mwezi mmoja ifikapo Septemba 30 iwe limekamilika na kutoa huduma kwa jamii,” amesema.

Aidha amezitaka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maji mkoani Mbeya kushirikiana katika kuhakikisha  chanzo cha maji cha Mto Kiwira kinatunzwa kwa kupanda miti rafiki na kuweka miundombinu  kulingana na ubora wa maji uliopo katika chanzo

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mbeya, (Mbeya -UWWAS)  Mhandisi ,  Gilbert Kayange amesema, mradi wa  mto Kiwira utazalisha lita  117 milioni  kwa siku na utahusisha shughuli za ujenzi wa banio, kulaza bomba kuu urefu wa kilometa 26.3.

Amesema mradi huo utagharimu zaidi ya Sh117 bilioni ambapo utekelezaji wake unaendelea na utakamilika Septemba 2025 hali ambayo itaboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

Mkazi wa Kiwira, Joel Mwaikambo ameomba Serikali kuharakisha utekelezaji wa mradi huo hususa vijana wazawa kunufaika na ajira kupitia mradi huo.