Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wizara: Ushawishi wa Tanzania kimataifa waongezeka

Muktasari:

  • Serikali inajivunia kuongezeka kwa uhusiano wa kimataifa,hususan kuongezeka kwa ushawishi wa Tanzania katika masuala ya kidiplomasia.

Dar es Salaam. Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema uhusiano wa nchi ya Tanzania kimataifa umezidi kuimarika.

Kuimarika huko kunatokana na utekelezaji wa sera ya mambo ya nje ambayo imeongeza mafanikio ikiwemo kuongeza ushawishi.

Hayo yamewekwa bayana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Kombo alipoongoza Menejimenti ya Wizara katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), kilichofanyika jijini Dodoma.

Kikao hicho kilichofanyika mwishoni mwa juma kilikua na lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu utendaji wa Wizara na hali ya ushirikiano wa kidiplomasia wa Tanzania.

"Mafanikio ya Serikali katika utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ni pamoja na kuimarika kwa uhusiano wa kimataifa,hususan kuongezeka kwa ushawishi wa Tanzania katika masuala ya kidiplomasia na hatua zinazochukuliwa kushughulikia changamoto zinazoikabili Wizara," amesema.

Aidha, katika kikao hicho, Balozi Kombo amewasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara, ikiwa ni pamoja na hali ya ushirikiano wa Tanzania na jumuiya za kikanda kama vile Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Vilevile amewasilisha hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maazimio ya Bunge yanayohusu sekta ya mambo ya nje na diplomasia ya uchumi.

Kwa upande wake, Kamati ya Bunge iliipongeza Wizara kwa kazi nzuri na kuishauri Wizara kuchukua hatua za makusudi kufanya maboresho zaidi ili Tanzania iweze kunufaika kikamilifu na ushirikiano wa kikanda na kimataifa.