Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wilaya zote nchini kuwa na intaneti mwakani

Dar es Salaam. Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesema ifikapo mwaka 2027, nyumba milioni moja zitakuwa zimefikiwa na intaneti ya kasi kubwa kupitia huduma ya ‘Fiber Connecter Bundle’.

Pia, wilaya zote nchini zitakuwa na huduma hiyo ifikapo Desemba mwakani.

Ahadi hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Shirika hilo, Mhandisi Peter Ulanga, alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari na kuongeza kuwa hadi Januari mwakani 2024, watakuwa wamefikisha huduma hiyo katika wilaya 100 na ifikapo Desemba, wawe wamefikia wilaya zote 139, baada ya kutatua baadhi ya changamoto.

Alisema huduma hiyo itawezesha wananchi wote nchi nzima kupata intaneti na wameshaanza kutoa huduma hiyo ambayo inapunguza gharama na huduma itafika maeneo mengi zaidi.

 Hata hivyo, katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2021/22, ilibaini utoaji usioridhisha wa huduma za intaneti uliofanywa na Shirika la TTCL katika baadhi ya hifadhi za Taifa na kukwamisha baadhi ya shughuli.

Shirika hilo pia linalalamikiwa kushindwa kutoa huduma shindani za mawasiliano ya simu za mkononi nchini.

Kutokana na ripoti hiyo ambayo Rais Samia Suluhu Hassan aliipokea Machi 29, mwaka huu, alishauri TTCL kujikita katika kusimamia mkongo wa Taifa ili kupunguza hasara ya kila mwaka.

Katika mkutano wake wa jana, Ulanga alisema maendeleo makubwa ya mawasiliano nchini, wao ndio mhimili mkuu na wanaamini uendelevu wao ndio uchumi wa kidijitali.

“Zipo changamoto, ikiwemo ya miundombinu haikuwa wezeshi sana, ndiyo maana kazi kubwa inafanyika ili kuongeza upatikanaji wa miundombinu ya mawasiliano nchi nzima, tunalibeba hilo na kuwawezesha wenzetu ili waweze kuitumia,” alisema.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile alisema sheria ya manunuzi ya umma ina changamoto na watu wasiofanya biashara hawawezi kujua ugumu wake.

Alisema mfano TTCL wakitaka kufanya uendelezaji wowote, wakianza mchakato wa manunuzi serikalini unaweza kuchukua hadi miezi sita, lakini kampuni nyingine zikihitaji kufanya uendelezaji kama huo ni rahisi.