Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wilaya ya Bagamoyo yawapoka wawekezajia eka 1,000 za ardhi

Muktasari:

NUKUU

"Baada ya kupata elimu ya ardhi kupitia simu na mikutano ya hadhara, wananchi wameelimika na wameanza kuhoji na hadi sasa zaidi ya eka 1,000 zime-rejeshwa vijijini.” Said Zikatimu

Dar es Salaam. Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo imerudisha zaidi ya eka 1,000 za ardhi zilizokuwa zimenunuliwa na wawekezaji kimakosa, baada ya wananchi kupata elimu ya kukabiliana na migogoro ya ardhi.

Akizungumza juzi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Said Zikatimu alisema elimu kupitia simu za mkononi inayotolewa na Taasisi ya C Sema kuhusu masuala ya ardhi, imesaidia ardhi hiyo kurejeshwa katika vijiji.

Alisema baadhi ya viongozi wa vijiji walikuwa wauza ardhi wakubwa kwa wawekezaji kinyume na sheria inayotaka wasiuze zaidi ya eka 50.

Alisema hivi sasa wananchi wanafahamu hatua za kuchukua inapotokea migogoro ya ardhi na hata vurugu kati ya wakulima na wafugaji imepungua.

Alisema kwa muda mrefu migogoro ya ardhi imekuwa kikwazo katika maendeleo na akashauri Serikali kuwa na mpango endelevu wa utoaji elimu ya ardhi ili kupata suluhisho. “Baada ya wananchi kuelimishwa kupitia ujumbe wa simu za mkononi, tatizo la migogoro ya ardhi limeanza kupungua, serikali izipe uwezo taasisi ziendelee kutoa elimu,” alisema.

Akizungumzia mradi huo, Ofisa Mtendaji wa Taasisi ya C Sema, Joel Kiiya alisema walikuwa wanatoa elimu ya uraia kupitia simu za mkononi na mikutano ya hadhara kwenye wilaya saba.

Alizitaja wilaya hizo kuwa ni Kahama, Tarime, Bagamoyo, Micheweni, Karagwe, Maswa na Mbeya Vijijini.

Alisema wananchi walihamasishwa kupima mashamba yao ili kukabiliana na migogoro ya ardhi.

Alisema mafanikio ya mradi huo katika kipindi cha miaka miwili ni kupungua kwa migogoro ya ardhi na ongezeko la utoaji wa vyeti vya kuzaliwa.

Alisema katika mradi huo wa miaka miwili, taasisi hiyo ilikuwa ikitoa elimu ya uraia iliyoambatana na masuala ya ardhi, mirathi na usajili wa vyeti vya kuzaliwa.

Alisema zaidi ya ujumbe 1,000 wa simu za mkononi ulitumwa kwa wananchi kwa lengo la kuwaelimisha masuala ya uraia.

Alisema mradi huo ulifadhiliwa na Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya Demokrasia (Undep).