Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wezi wavunja kanisa KKKT Hai, waiba mamilioni

Muktasari:

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linaendelea na uchunguzi ili kubaini watu waliovunja ofisi ya Mhasibu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Nronga, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na kuiba zaidi ya Sh3 milioni za sadaka na kompyuta mpakato.

Hai. Watu wasiojulikana wamevunja ofisi ya Mhadibu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Nronga, Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro na kuiba zaidi ya Sh3 milioni za sadaka na kompyuta mpakato yenye thamani ya Sh780,000.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Januari 8, 2024 na uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Akielezea mazingira ya tukio hilo, Kamanda Maigwa amesema wezi hao walivunja kitasa cha ofisi ya mhasibu wa kanisa, kuiba fedha na kompyuta na kutokomea navyo kusikojulikana.

"Januari 8, 2024 saa 1:45 asubuhi katika kijiji cha Nronga Machame, Kanisa la KKKT usharika wa Nronga, kilivunjwa kitasa cha ofisi ya mhasibu wa Kanisa na kuibiwa fedha Sh3.01 milioni na kompyuta mpakato moja aina HP, na mtu au watu wasiofahamika.

"Januari 7, 2024 baada ya kukamilika ibada ya siku Jumapili, mhasibu wa kanisa alihesabu fedha za makusanyo mbalimbali zaidi ya Sh3 milioni na kuzihifadhi ofisini kwake sehemu tofautitofauti, ndani ya kabati, juu ya meza na kwenye kapu la kuhifadhia sadaka," amesema.


Aidha kamanda amesema, ofisi hiyo iko umbali wa mita 56 kutoka mahali lilipo kanisa na kasiki la kuhifadhia sadaka halikuvunjwa, hivyo upelelezi kuhusiana na tukio hilo bado unaendelea ili kuwakamata wahusika.

Akupotafutwa Mkuu wa Jimbo la Hai, Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT, Mchungaji  Biniel Mallyo kuhusiana na tukio hilo, amesema kwa sasa hawezi kulizungumzia kwa undani kwa kuwa zipo hatua ambazo zinaendelea kuchukuliwa na vyombo vya usalama.

"Kuna taratibu zinaendelea hivyo hatuwezi kuzungumza chochote kwa sasa kuhusiana na tukio hilo, lakini mwisho wa siku tutaliweka vizuri na taarifa zitatolewa," amesema.