Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

WCF yatakiwa kusajiri watumishi kada zote

Katibu Mkuu Wizara ya kazi, ajira, vijana na wenye ulemavu Cyprian Ruhemeja  akizungumza katika kikao Cha Baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) kinachoendelea mjini Morogoro. Lilian Lucas

Muktasari:

  • Katika kuhakikisha wafanyakazi wa kada zote wanapata huduma wanazozikosa WCF inatakiwa kuwafikia kwa wakati na haraka.

Morogoro. Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Cyprian Ruhemeja ameuagiza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), kuona haja ya kusajili watumishi kutoka kada zote za umma na binafsi ili waweze kupata huduma wanazozikosa.

Ruhemeja amesema hayo Oktoba 20, 2023 wakati akifungua kikao cha Baraza la wafanyakazi wa WCF kinachofanyika mkoani hapa ambapo amesema ni vema viongozi wakafanya jitihada na kuhakikisha wanasajili watumishi wote hadi ifikapo mwakani mwezi Juni.

Amesema mfuko huo ni kwa ajili ya kuwasaidia watanzania wote katika masuala mbalimbali ikiwemo wanapopata ajali na changamoto nyingine za kimaisha na kwamba unahitaji kutunzwa na kulinda na kuleta dhana kamili ya kuweza kuwarishisha vizazi na vizazi.

Aidha amesema Serikali kupitia mfuko huo imeweka utaratibu wa kumsaidia mtu anayefanya kazi Serikali kuu na sekta binafsi wakati yupo kazini na baada ya kutoka kazini lakini maana ya mfuko huo haitatimia kama hakutakuwa na idadi kamili ya waliosajiliwa kulingana na idadi ya watumishi waliopo nchini.

“Mnaniambia mpaka sasa mmesajili asilimia 70, na mnalenga kusajili watu 3000 kila mwaka, hapo ni bado sana, ongezeni nguvu na msajili wafanyakazi ili wote wanufaike,” amesema Ruhemeja.

Hata hivyo amewasisitiza kutosahau majukumu yao ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwa wabunifu na kutoka elimu kwa jamii ili waifahamu WCF na umuhimu wake kwao kwa sababu asilimia 80 ya watumishi hawaifahamu wanabaki kuuliza tuu.

Mkurugenzi Mkuu wa WCF ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi Henry Mduma ameahidi kuimarisha mfuko huo ukiwa na taarifa za kutosha za wafanyakazi ambao watapata huduma.

Mduma amesema mpaka sasa wana jumla ya asilimia 92 ya waajiri waliosajiliwa kwenye taarifa zao huku asilimia 100 wakiwa ni waajiri wakubwa na asilimia 92 wakiwa ni waajiri wa kati.