Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Mkenda: Mtaala mpya kutoa wahitimu wenye ujuzi

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda (wa kwanza kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima (wa pili kushoto) wakiangalia vifaa katika moja ya Maabara za Sayansi katika Chuo cha Ualimu Butimba jijini Mwanza. Picha na Damian Masyenene.

Muktasari:

Tanzania ina Vyuo vya Umma 35 vya Ualimu vyenye zaidi ya wanafunzi 22, 000 huku akikadiriwa kuwa takriban wanafunzi 11,000 wanahitimu ngazi mbalimbali za ualimu nchini.

Mwanza. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema maoresho ya mitaala ya elimu nchini utasaidia kuzalisha wahitimu wenye ujuzi na maarifa katika fani wanazosomea.

Akizungumza jijini Mwanza Aprili 25, 2023 wakati wa hafla ya kuzindua majengo mapya na yaliyokarabatiwa ya Maabara za Fikzikia, Kemia, Bailojia, Tehama na Maktaba katika Chuo cha Ualimu Butimba, Profesa Mkenda amesema wahitimu hao pia watakuwa na uwezo wa kujiajiri na kutengeneza ajira kwa wengine.

Amesema ili kufanikisha lengo hilo, Serikali inafanya mageuzi katika eneo la Elimu ya Ualimu nchini kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya ikiwamo Maabara za Sayansi na Tehama, kugawa vishikwambi na kusambaza mkongo wa Taifa wa intaneti katika vyuo 35 vya ualimu nchini.

Majengo yaliyozinduliwa Chuo cha ualimu Butimba yajengwa na kukarabatiwa kwa gharama ya zaidi ya Sh467.6 milioni kupitia Mradi wa kuendeleza Elimu ya Ualimu (TESP) unaofadhiliwa na Serikali ya Canada.

“Tuko kwenye hatua za mwisho za kupokea maoni ya wadau kuhusu mtaala mpya utakaoongeza masomo ya kilimo, ufugaji, uvuvi, ushonaji na mengine, lengo ikiwa ni kuwawezesha wahitimu kuwa na ujuzi, maarifa, uwezo na tayari wa kujitegemea,” amesema Profesa Mkenda.

Amesema uwekezaji na mabadiliko hayo ni jitihada za Serikali za kuchochea mabadiliko chanya katika eneo la ualimu unaoenda sambamba na ugawaji wa vishikwambi kwa walimu kuwawezesha kufundisha kisasa na kupunguza gharama za kuchapisha vitabu kwa sababu vitapatikana kwa njia ya mtandao.

Mratibu wa Mradi wa TESP, Cosmas Mahenge amesema tayari wamesambaza mkongo wa Taifa wa intaneti katika vyuo 15 kwa lengo la kurahisisha ufundishaji ambapo; na ifikapo Juni 30, 2025 vyuo vyote 35 vya ualimu vitafikiwa.

Amesema kufikia muda huo, wakufunzi zaidi ya 1,300 watakuwa wamepata mafunzo ya ualimu, ujenzi wa umahiri, Tehama na utengenezaji wa mfumo wa kidigitali wa kusahihisha mitihani.

Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo kutoka Wizara ya Elimu, Huruma Mageni amesema ukarabati wa miundombinu ya Chuo cha Ualimu Butimba umezesha maabara za Sayansi na Tehama za chuo hicho kikongwe nchini kuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi 130 kila moja kwa wakati mmoja.

Amesema utekelezaji wa miradi ya aina hiyo pia umefanyika katika vyuo sita vya ualimu vya Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpwapwa, Patandi na Tukuyu kwa gharama ya zaidi ya Sh4.1 bilioni.