Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wazimbabwe watatu kortini wakidaiwa kuiba Sh51.2 milioni Kariakoo

Washtakiwa watatu ambao ni raia wa Zimbabwe, wakiwa chini ya ulinzi wa askari kanzu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kusomewa shtaka la wizi.

Muktasari:

  • Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 4, 2024, Mtaa wa Manyema na Mhonda, uliopo Kariakoo.

Dar es Salaam. Raia watatu wa Zimbabwe, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shitala la wizi wa Sh51.2 milioni.

Washtakiwa hao ni Patricia Marufu (47), Sunungurai Makombo (46) na Melusi Dube (53) na wote makazi yao ya muda ni Manzese, Wilaya ya Ubungo.

Marufu na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo, leo Julai 15, 2026 na kusomewa kesi ya jinai na wakili wa Serikali Mwandamizi, Leonard Chalo.

Chalo amewasomea shtaka lao, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aziza Temu.

Alidai washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 4, 2024, mtaa wa Manyema na Mhonda, uliopo Kariakoo, Wilaya ya Ilala.

Inadaiwa siku hiyo, washtakiwa kwa pamoja wakiwa eneo hilo waliiba Sh51.2 milioni, mali ya Safina Othuman.

Hata hivyo, baada ya kusomewa shtaka hilo walikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa umekamilisha upelelezi.

“Mheshimiwa hakimu, uchunguzi wa kesi hii umekamilika, hivyo tunaomba mahakama yako itupangie tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea hoja za awali washtakiwa hawa,” alidai wakili Chalo.

Kuhusu dhamana, wakili Chalo alidai hana pingamizi ila aliomba mahakama itoe masharti kwa mujibu wa sheria.

Hakimu Temu, alitoa masharti matatu ambayo ni kila mshtakiwa anatakiwa kuwasilisha mahakamani hapo fedha taslimu Sh8.5 milioni. Pia, kila mshtakiwa anatakiwa awe na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria watakaosaini bondi ya Sh5 milioni kila mmoja.

Sharti lingine, washtakiwa hao  wanatakiwa kusaini bondi ya Sh5 milioni.

Baada ya kutoa masharti hayo, hakimu Temu aliahirisha kesi hadi Julai 27, 2026 kwa ajili ya jamhuri kuwasomewa hoja za awali, washtakiwa hao.

Washtakiwa wameshindwa kutimiza masharti ya dhamana   hivyo wamepelekwa rumande.