Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wazee, wenye ulemavu wakumbukwa

Muktasari:

  • Msaada huo umetolewa kupitia programu ya Tulia Trust Mtaani Kwetu kwa lengo la kurejesha tabasamu kwa kaya zisizojiweza na zinazoishi katika mazingira magumu, ikiwa ni shamrashamra za  sikukuu za mwisho wa mwaka.

Rungwe. Wazee na watu wenye ulemavu wilayani hapa wameshindwa kujizuia na kububujikwa  machozi, baada ya kukabidhiwa  chakula na  fedha kwa ajili ya  kusherehekea  sikukuu za mwisho wa mwaka.

Mahitaji hayo yametolewa leo Jumanne Desemba 26, 2023 kupitia program ya Tulia Trust mtaani kwetu, inayoendeshwa na Taasisi ya Tulia Trust iliyolenga kusaidia kaya 13 zisizojiweza wakiwepo wazee na watu wenye ulemavu.

Awali akipokea msaada huo kikongwe, Never Kisuru (80) ameeleza kuwa, hakutegemea kupata msaada huo wa chakula na kuungana na Watanzania wengine kusherehekea sikukuu kwa kula na kunywa.

 “Mimi ni mjane hapa nilipo sina msaada lakini ninyi vijana Mungu kawagusa mmetumbuka hata tuliosahaulika kwenye jamii, tunawaombea kwa Mungu mkajazwe na kuongezeka,” amesema.

Kisuru ameomba taasisi hiyo isiishie kwao tu bali iwakumbuke na wahitaji wengine, kwani wilayani Rungwe wako wengi wenye changamoto za mahitaji mbalimbali.

Kwa upande wake, Ambele Wilfredy mwenye ulemavu, amesema, “Binasfi niishukuru sana hii taasisi kwani licha ya mahitaji pia nimejengewa makazi yangu ambayo yalikuwa hatarishi sambamba na msaada wa baiskeli ya kitimwendo,  ambayo inaniwezesha kutoka sehemu moja kwenda nyingine,” amesema.

Naye Ofisa habari na mawasiliano wa taasisi hiyo, Joshua Mwakanolo amesema kuwa mahitaji hayo yaliyotolewa kwa makundi ya wazee na walemavu yana thamani ya Sh3 milioni.

“Kupitia program hii hatutaishia kutoa mahitaji ya chakula pekee bali kukarabati na kujengwa makazi ya vikongwe, walemavu ambayo yako hatarini,” amesema.

Amesema kupitia program hiyo kaya 13 zilizofikiwa zilibainika kwenye siku saba za kukimbiza bendera upendo, uwajibikaji iliyokimbizwa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.