Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wazazi watakiwa kuacha kuficha watoto wenye ulemavu

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Wazazi wametakiwa kutowaficha watoto wao wenye ulemavu na badala yake wawapeleke shule ili kuwajengea uwezo wa kumudu maisha yao ya baadaye.

Dar es Salaam. Wazazi wametakiwa kutowaficha watoto wao wenye ulemavu na badala yake wawapeleke shule ili kuwajengea uwezo wa kumudu maisha yao ya baadaye.

  

Wito huo umetolewa na Mwanzilishi na Mlezi wa Kituo cha Elimu na Malezi ya watoto cha Mwanangu Special Day Care & Rehabilitation Centre kilichopo Vikindu, Janet Manoni, wakati wa mkutano uliowakutanisha wazazi na wadau kujadili yaliyojiri mwaka huu, na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto kwa mwaka ujao.

Katika mkutano huo wazazi waliibua hoja mbalimbali ikiwemo watoto wao wananyanyapaliwa katika shule nyingi na hata zile zinazowakubali, hazina miundombinu rafiki kwa watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali.

Akijibu hoja hizo, Janet amewasihi wazazi kutokata tamaa kwani serikali inasisitiza kutokuwepo na kikwazo chochote katika upatikanaji wa elimu kwa watoto wote hivyo wazazi wawapeleke shuleni.

“Hebu tuachane na tabia za kufungia watoto ndani,
kuwaficha na kuwatenga na wenzao kwani kwa kufanya hivyo tunawanyima haki zao za msingi na pia ni kuvunja
haki za watoto na haki za binadamu kwa ujumla.

“Tunayo mifano halisi kwa watoto walio hapa mbele yetu ambao walipoletwa hapa kwa mara ya kwanza
hawakuweza kujimudu kwa lolote lakini ndani ya mwaka mmoja, mnaona maendeleo yao, wanaweza kufanya mambo yao binafsi kama usafi, michezo na pia darasani wamepiga hatua kubwa.

Hebu tushirikiane kuwaibua watoto walio mitaani na tujitoe kuwasaidia ili wapate elimu,” amesisitiza Janet.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Club ya Lion tawi la Uhuru Dar es Salaam, Sukaina Esmail, akikabidhi vifaa mbalimbali vilivyotolewa na taasisi yake, amepongeza juhudi zinazofanywa na kituo hicho kuwapa elimu watoto hasa wenye ulemavu.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na magodoro, mashuka, vyandarua, mito, maziwa, sukari, vitakasa mikono, dawa za meno nk, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu wa masomo kwa mwaka 2022.
“Tunatambua changamoto zilizopo katika kulea mtoto
mwenye ulemavu. Wapo wazazi wanaokata tamaa kwa sababu ya umaskini au vikwazo vinavyosababishwa na
jamii tunamoishi hivyo uwepo wa shule kama hizi ni mkombozi sio tu kwa mzazi bali pia hata taifa kwani kila mtoto ana haki ya kupata elimu,” amesema Sukaina.

Ameongeza kuwa, wanatambua na kuunga mkono kituo hicho kinavyoshughulika na watoto wenye kansa, kichwa kikubwa na mgongo wazi ili kuendeleza ustawi wa watu na dunia.

Kwa upande wao, wazazi wameshukuru wadau
wanaojitolea kushirikiana na serikali katika kulinda haki za watoto kama upatikanaji wa elimu na huduma za afya.