Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili wauawa shambani Kilosa Morogoro

Morogoro. Ikiwa imepita wiki moja tangu mtumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa alipouawa akiwa nyumbani kwake, Julai 23 tukio jingine la mauaji limetokea wilayani humo ambapo watu waili wameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha katika matukio mawili tofauti.

Akizungumia matukio hayo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Hassan Maya amewataja watu waliouawa kuwa ni Shabani Haruna (40), na Benson Mwakasanga (48), ambao wote wameuawa nyakati za usiku wakiwa kwenye mashamba yao, kwa kukatwa vitu vyenye ncha kali kichwani.

Kwa upande wa marehemu Haruna, Kaimu Kamanda huyo amesema kuwa polisi wameanza uchunguzi na mpaka sasa mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Abdallah Chande (40), anashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi kuhusu tukio hilo, na kwamba bado jitihada za kuwatafuta watuhumiwa wengine zinaendelea.

Amesema kuwa mwili wa marehemu umeshafanyiwa uchunguzi wa kidaktari na tayari ndugu wameshakabidhiwa mwili huo kwa ajili ya maziko.

Na kwa upande wa tukio la Mwakasanga, Kamanda Maya amesema uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo unaendelea, huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano ili kufanikisha kupatikana kwa wahusika wa mauaji hayo.

Kaimu Kamanda huyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano, ili kufanikisha kupatikana kwa wahusika wa mauaji hayo.