Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili wauawa kwa kuchomwa moto, wakituhumiwa matukio ya uvamizi

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi

Muktasari:

  • Vijana wawili wameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira wakituhumiwa kujihusisha na matukio ya uvamizi.

Shinyanga. Jeshi la Polisi mkoani hapa, linaendelea na uchunguzi wa tukio la wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaua vijana wawili kwa kuwachoma moto, wakituhumiwa kwa matukio ya uvamizi.

 Vijana hao waliuliwa na wananchi wenye hasira katika Kijiji cha Lyandu Wilaya ya Shinyanga na kisha kuteketeza kwa moto nyumba aliyokuwa amejificha mtuhumiwa mmoja.

Akizungumza kuhusiana na tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga,  Janeth Magomi amesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo la wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaua vijana wawili katika matukio mawili, wakiwatuhumu kufanya uvamizi.

Kamanda Magomi amewataja vijana wanaotuhumiwa kufanya uvamizi katika Kijiji cha Lyandu ambao wameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi kuwa ni Bahati Dotto(36) na mtuhumiwa mwingine aliyefahamika kwa jina la Emmanuel aliuawa katika  Kijiji cha Bugayambelele.

Kutokana na tukio hilo, Kamanda Magomi amewataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani kitendo hicho hakitakiwi na kuahidi kufanya uchunguzi ili kuwabaini wote waliohusika na tukio hilo.

Akizungumzia tukio hilo leo Juni 06,2024, Mwenyekiti wa Mtaa wa Iwelyangula Kata ya Chamaghuha,  Robarth Mnyeleshi amesema aliona umati mkubwa wa wananchi wakiwa kwenye nyumba alipokuwa amejificha kijana Bahati Dotto(36)ambaye alichomwa moto kisha nyumba hiyo pia kuteketezwa kwa moto.

Amesema wananchi waliotekeleza mauaji hayo ni kutoka Kijiji cha Lyandu ambao walifika katika Mtaa wake wakiwatafuta watuhumiwa na kufanikiwa kumpata mmoja ambaye walimchoma moto baada ya kuwaeleza mtuhumiwa mwingine alipo.

Akisimulia tukio hilo mmoja wa familia ambayo nyumba yao imechomwa moto,  Ester Ngubu amesema walikuwa ndani usiku, wakasikia sauti za watu nje wanaongea baada ya kufungua mlango walipowauliza wakadai wanamtafuta Bahati ayejificha kwenye nyumba hiyo.

Amesema kutokana na hasira za wananchi hao kutaka kuchoma moto nyumba hiyo ndipo aliomba msaada wa kumtoa ndani bibi yake ambaye alikuwa ameshikiliwa na kijana aliyekuwa akitafutwa  akidai wanakufa wote na kufanikiwa kumtoa kisha wananchi wakachoma moto nyumba.

Mkazi wa eneo hilo,  Jackson Peter  amesema kitendo hicho  ni kinyume cha sheria kutokana na kuharibu mali ya watu wasiokuwa na hatia kwa kuchoma moto nyumba jambo ambalo linakiuka haki za binadamu.