Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili mbaroni tuhuma za kumuua mwenyekiti wa UVCCM Makongorosi

Aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Machinjioni Kata ya Makongorosi Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya Michael Kalinga enzi za uhai wake.

Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) ,Tawi la Machinjioni, Kata ya  Bwawani  Michael Kalinga (36) mkazi wa Makongorosi wilayani Chunya .

Kaimu Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Mbeya,Wilbert Siwa akizungumza na vyombo vya habari  leo Jumatano, Desemba 4, 2024  amesema  tukio hilo lilitokea usiku wa Jumatatu,  Desemba  2, 2024 saa 5.30 usiku eneo la Mianzini  Kata ya Mkola.

Amesema mwenyekiti huyo ameuawa kwa kupigwa na kitu butu sehemu ya utosini kwake kisha mwili wake kutelekezwa umbali wa mita 250 kutoka barabara ya Makongorosi kuelekea Lupa tingatinga.

"Baada ya kutokea mauaji hayo Jeshi la Polisi lilifanya msako ambapo  jana Desemba 3, 2024 huko Mji wa  Mlowo, Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe tulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na pikipiki iliyokuwa ikitukiwa na marehemu yenye namba za usajili MC 464 ELL,"amesema Siwa.

Siwa amesema watuhumiwa hao (majina yamehifadhiwa) baada ya kuhojiwa na wamekiri kuhusika na mauaji ya mwenyekiti huyo  na kisha  kupora pikipiki aliyokuwa akitumia.

Amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa baada ya uchunguzi kukamilika.

Wakati Jeshi la Polisi likieleza kuwashikilia watuhumiwa wawili Baba mzazi wa marehemu Michael Kalinga (36), Adalas Mwijagege (65) ameomba sheria ichukue mkondo wake.

Amesema kikubwa anashukuru kazi iliyofanywa na Jeshi la Polisi kufanikisha kwa watuhumiwa hao wawili pamoja na vielelezo ikiwepo pikipiki ya marehemu kukamatwa.

Pia ameomba wafikishwe mahakamani kwa hatua zaidi.