Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili mbaroni kwa tuhuma za mauaji, maiti yaokotwa shambani

Mwili wa mwanamke aliyekutwa ameuawa na watu wasiojulikana kijiji cha Bunambiyu Wilaya ya Kishapu.

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya Hollo Ruchanganya (60) kisha mwili wake kutupwa kwenye shamba la mahindi.

Shinyanga. Mwili wa mwanamke mwenye umri wa miaka (60) aliyefahamika kwa jina la Hollo Ruchanganya umekutwa umetupwa katika shamba la mahindi karibu na makazi yake katika Kijiji cha Bunambiyu Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga, tukio ambalo limezua taharuki kwa wananchi wa kijiji hicho.

Tukio hilo limetokea jana Aprili 3, 2026 ambapo mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake usiku akiongozana na mtu asiyefahamika, baada ya mgeni huyo kufika nyumbani kwake na kujitambulisha kuwa anatoka Kijiji cha Sanga Wilayani Kwimba na kuomba kupelekwa kwa mganga wa jadi Ng’wana Masanja ambaye ni ndugu wa marehemu.

Mtoto wa marehemu Kashinje Selemani, amesema baada ya kupata taarifa alikwenda nyumbani na kukuta tukio hilo kisha kuelezwa kuwa alifika hapo nyumbani mtu ambaye hawamfahamu na kuzumgumza na mama yake kisha kuondoka naye.

Amesema Hollo ambaye kwa sasa ni marehemu, alikubali kuongozana na mgeni huyo kwa lengo la kumpeleka kwa mganga wa jadi ambaye ni mama yake mdogo na marehemu, hata hivyo hakurejea tena nyumbani hadi mwili wake ulipogunduliwa asubuhi na ndugu yake ukiwa shambani.

Kwa upande wake kaka wa marehemu Anderson Malashi amesema alipofika kwenye familia hiyo majira ya saa tatu usiku alidai anatafuta mganga wa kuwatibu mapacha na kwamba ameelekezwa kwa mama huyo ili ampeleke ndipo hakurejea tena nyumbani.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Bunambiyu Boniface Zengo amesema alipigiwa simu kuelezwa juu ya tukio hilo na kwenda eneo hilo la tukio, ambapo baada ya kuelezwa na watoto wa familia hiyo na kufanya ufuatiliaji kisha kupata mwili huo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Janeth Magomi, amesema tayari watu wawili wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo huku uchunguzi ukiendelea kubaini ukweli zaidi.

Amesema kuwa tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina huku akionya kuwa bado kuna baadhi ya watu wanaoendeleza vitendo hivyo hatarishi, vinavyohatarisha maisha ya wengine na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi halitavumilia matukio ya mauaji yanayotokana na imani hizo.