Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waumini watakiwa kukamilisha kwaresma

Muktasari:

  • Katika kuadhimisha kifo na mateso ya bwana wetu Yesu Kristu, Jimbo Katoliki la Moshi limeshangaa kuona baadhi ya Wakristu wakiwa kwenye maeneo mbalimbali wakila chips na nyama wakati wa siku ya Ijumaa kuu.

  

Moshi. Katika kuadhimisha kifo na mateso ya bwana wetu Yesu Kristu, Jimbo Katoliki la Moshi limeshangaa kuona baadhi ya Wakristu wakiwa kwenye maeneo mbalimbali wakila chips na nyama wakati wa siku ya Ijumaa kuu.

Akifunga Misa ya Ijumaa kuu iliyofanyika katika Parokia ya Kristu Mfalme,Jimbo katoliki la Moshi,Paroko wa Parokia hiyo Evans Mavumilio amewataka waumini wa kanisa hilo kuacha  kupita huko na huko wakati mfungo wa siku 40 haujaisha.

"Leo tuliandamana njia ya msalaba kutoka kanisa katoliki Korongoni kuja Kanisa kuu lakini tumeshangaa kweli na hata Baba Askofu ameshangaa kuona chips ,nyama na yale maji ya dhahabu(bia) na watu wanatumia sasa tukajiuliza hili ni kundi la wapi wakati sisi wakatoliki tumefunga na ni Ijumaa kuu,"

"Naomba tukumbushane sisi wakatoliki bado tunaendelea na mfungo ,tusiende kufungulia na tusishindwe na vitu vidogovidogo wakati wa mfungo huu wa siku 40,"amesema Padre Mavumilio

Pamoja na mambo mengine amesema Jimbo hilo limeanza leo Novena ya huruma ya Mungu ya  siku 9 kwa ajili ya kuziombea nchi za Russia na Ukraine zikomeshe vita vinavyoendelea vya umwagiji wa damu.



"Baba Askofu anatualika kwa kipindi chote kusali Novena ya siku 9 kuombea nchi za Russia na Ukraine ili Mwenyezi Mungu aweze kukomesha vita vya umwagaji mkubwa  wa damu vinavyoendelea kwa sasa,"amesema Padre Mavumilio