Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watumishi wa umma walainishiwa kupata mikopo

Muktasari:

  • Mikopo hiyo inalenga kupunguza usumbufu na kuongeza ufanisi katika mchakato wa upatikanaji wa mikopo kwa kutumia teknolojia, hatua inayotajwa kusaidia kuongeza tija kwa watumishi wa umma.

Dar es Salaam. Benki ya Stanbic Tanzania imezindua rasmi huduma mpya ya mkopo wa kidigitali kwa watumishi wa umma, ujulikanao kama eMkopo, kupitia mfumo wa Serikali wa Watumishi Portal.

Huduma hiyo, ambayo inalenga kuleta mapinduzi katika utoaji wa huduma za kifedha, inawawezesha watumishi wa umma kuomba mkopo wa hadi Sh200 milioni na kuurejesha kwa kipindi cha hadi miaka tisa, bila kufika tawi la benki.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Stanbic Bank, Emmanuel Mahondanga, alisema eMkopo ni hatua kubwa katika kukuza ujumuishwaji wa kifedha nchini.

“Kwa kuunganishwa na mfumo wa Watumishi Portal, tunarahisisha mchakato mzima wa upatikanaji wa mikopo kwa njia ya haraka, salama na rafiki kwa mtumiaji,” alisema Mahondanga.

Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa Mauzo na Upatikanaji Wateja wa benki hiyo, Priscus Kavishe, alisema huduma hiyo ni matokeo ya ushirikiano kati ya sekta binafsi na ya umma.

“Kupitia jukwaa rasmi la Serikali – Watumishi Portal – mtumishi wa umma anaweza kuomba mkopo kidigitali na kuanza marejesho kwa masharti nafuu,” alisema Kavishe.

Huduma hiyo inalenga kupunguza usumbufu na kuongeza ufanisi katika mchakato wa upatikanaji wa mikopo kwa kutumia teknolojia, hatua inayotajwa kusaidia kuongeza tija kwa watumishi wa umma.