Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watu 22 mbaroni kwa tuhuma za mauaji Mbeya

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, Urlich Matei akizungumza na waandishi wa habari

Muktasari:

Matukio ya mauaji yameonekana kushamiri maeneo mbalimbali nchini huku Mkoa wa Mbeya ukiwa miongoni mwa Mikoa iliyoripotiwa kwa vitendo hivyo.

Mbeya. Kufuatia kuwepo kwa wimbi la matukio ya mauaji jijini Mbeya, Jeshi la Polisi mkoani humo limewatia nguvuni watu 22 kwa tuhuma za kuhusika na vitendo hivyo, huku likitoa mwelekeo wa namna ya kumaliza matukio hayo.

Hivi karibuni kumekuwapo na matukio kadhaa ya mauaji, yakiwamo ya aliyekuwa mwalimu mstaafu, Edward Ndonde aliyeuawa na mwanaye Mussa Edward Januari 12, Justine Namwinga aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Hasanga naye aliuawa na watu wasiojulikana Januari 31 huku Gloria Kibira aliyekuwa Afisa Ustawi mwandamizi aliyekutwa amenyongwa nyumbani kwake Februari 3 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Februari 8, 2022, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, Urlich Matei amesema katika operesheni na msako mkali uliofanywa maeneo mbalimbali jijini humo, limewakamata watuhumiwa hao kwa makosa ya kuhusika na matukio hayo.

Amesema katika upelelezi uliofanywa na Jeshi hilo, umebaini vyanzo vya mauaji hayo ni ulevi, wivu wa kimapenzi, imani potofu (ramli chonganishi), migogoro ya ardhi, kuwania mali na kujichukulia sheria mkononi.

"Watuhumiwa 16 kati ya 22 wamefikishwa mahakamani na wengine watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa mashauri yao kukamilika" amesema Matei.

Matei amesema ili kukomesha matukio hayo, wananchi wanapaswa kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kuwafikisha watuhumiwa Polisi, viongozi wa serikali za Mitaa watendaji wa Kata kutumia mabaraza ya usuluishi kutatua migogoro ya ardhi na kuwatumia wataalamu waliopo katika kamati za ulinzi na usalama kutoa elimu ya namna ya kudhibiti msongo wa mawazo.

Mmoja wa wananchi katika mtaa wa Sokoine, Herieth Magimba amesema kwa sasa hali inatisha kutokana na mauaji yanayoripotiwa akiwaomba wananchi kumrudia Mungu na kutubu dhambi akisema kuwa Serikali pia iongeze ulinzi maeneo mbalimbali.

"Kila siku tunasikia mauaji hadi sisi tunaogopa, tuna familia zetu Mikoa mingine hivyo tunabaki na wasiwasi kubwa kwa sababu hawa wanaowaua hadi wazazi na ndugu zao wakikosa wa kuua watatuua sisi au watoto wetu, Polisi waimarishe ulinzi maeneo mengi" amesema Herieth.