Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watatu kortini wakidaiwa kusafirisha kilo 145 za mirungi

Mshtakiwa Said Ndomboloa(wa kwanza kulia) alifuatilia wa na Amor Seiph( katikati) na Hamisi Ndomboloa, wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu baada ya kusomewa kesi ya kusafirisha mirungi kilo 145. Picha na Hadija Jumanne

Muktasari:

  • Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa yao Julai 18, 2019, eneo la Gongo la Mboto na Posta.

Dar es Salaam. Said Ndomboloa na wenzake wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina mirungi zenye uzito wa kilo 145.20.

Mbali na Ndombokoa, washtakiwa wengine ni Hamisi Ndomboloa na Amor Seiph.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumatatu, Februari 17, 2025, na kusomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Asiat Mzamiru, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swallo.

Wakili Mzamiru amedai kuwa Julai 18, 2019, eneo la Gongo la Mboto, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa kilo 105.17, kinyume cha sheria.

Shtaka la pili, Julai 18, 2019, katika ofisi za Posta zilizopo wilaya ya Ilala, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kusafirisha kilo 40.03 za mirungi, kinyume cha sheria.

Baada ya kusomewa mashtaka yao, upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika na wapo katika hatua za kusajili taarifa na nyaraka muhimu Mahakama Kuu.

Baada ya kueleza hayo, hakimu Swallo ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 3, 2025 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayowakabili hayana dhamana.