Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watanzania wawili watoweka eneo la mashambulizi Israel

Balozi wa Tanzania nchini Israel, Alex Kallua.

Muktasari:

  • Watanzania wawili wanaoishi katika eneo lililokumbwa na mashambulizi nchini Israel kutoka kwa vikosi vya Hamas hawajulikani walipo kwa mujibu wa Balozi Kaullua.

Dar es Salaam. Watanzania wawili wanaoishi katika moja ya eneo lililokubwa na mashambulizi nchini Israel kutoka kwa vikosi vya Hamas hawajulikani walipo.

Ubalozi wa Tanzania nchini Israel unasema hauna mawasiliano na raia wawili wa Tanzania ambao wanakaa eneo la Kusini mwa Israel ambalo limeshuhudiwa mapambano baina ya wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas na jeshi la Israeli.

Kwa mujibu wa BBC, Balozi wa Tanzania nchini Israel, Alex Kallua amesema kuwa mpaka leo Jumatatu asubuhi, ubalozi huo umekuwa na mawasiliano na Watanzania takribani 350 waliopo nchini humo kasoro raia hao wawili ambao ni wanafunzi.

”Tunaendelea kuwafuatilia Watanzania wawili ambao ni wanafunzi waliokuwa wanafanya mafunzo kwa vitendo Kusini mwa Israel.

“Tunafanya jitihada za kuwapata kwanza ili kufahamu walipo na hali zao,” amesema Balozi Kalua.

Aidha ameongeza kuwa wanafunzi wengine takribani 260 kati ya Watanzania zaidi ya 350 wako salama katika maeneo mbalimbali nchini humo na wamekuwa na mawasiliano na ubalozi.

Pia amesema kuwa wanaendelea kufuatilia hali ya usalama nchini humo ili kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa salama.

”Tunafuatilia kwa karibu na tunaendelea kupata taarifa kutoka mamlaka za Israel kuhusu hali ilivyo. Tunaendelea kufuatilia na kuwaeleza waliopo hali ilivyo,” alisema balozi huyo.


Imeandaliwa na Victor Tullo kwa msaada wa mashirika.