Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watanzania milioni tano kunufaika na bandari Kilwa

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega akielekeza jambo, wakati alipotembelea eneo linapojengwa bandari

Muktasari:

  • Zaidi ya Sh260 bilioni, zitatumika katika mradi mkubwa wa bandari inayojengwa katika eneo la Kilwa Masoko, mkoani Lindi.

Kilwa. Wananchi wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi, watanufaika na mradi mkubwa wa bandari ya kisasa ya uvuvi, ambayo inaojengwa katika Halmashauri ya Kilwa, mjini Kilwa Masoko, Mkoa wa Lindi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ameyasema hayo leo Alhamis Septemba 14, 2023 wakati alipotembelea na kuona maendeleo ya ujenzi huo, huku akisema Sh260 bilioni zitatumika katika ujenzi huo.

Ulega ameendelea kusema kuwa, hadi sasa mradi huo umetoa ajira 30,000 na kwamba wazawa ndiyo wanapewa kipaumbele hasa kwa zile kazi ambazo hazihitaji utaalamu.

"Pia bandari hii itakapokamilika, haitanufaisha wakazi wa Lindi pekee, bali itawasaidia watu wote wa maeneo yote ya ukanda wa pwani ikiwemo mikoa ya Pwani, Zanzibar na Mtwara. Zaidi ya watanzania million 5 watanufaika kutokana na shughuli za uvuvi, usindikaji wa samaki na biashara ndogondogo," amesema.

Kwa mujibu wa Waziri Ulega, mradi huo unatarajiwa kumalizika ifikapo 2025 na kwamba hadi sasa ujenzi wake umefikia asilimia 22.

Baadhi ya wananchi wanaoishi katika eneo la mradi wamesema kuwa mradi huo utawanufaisha wananchi kwa kupata ajira na kufanya biashara mbalimbali.

Mmoja wa wananchi hao ni Hafidhi Saidi, ambaye amesema fursa watakazozipata baada ya mradi kukamilika, zitasaidia kuinua kipato situ cha watu wa Lindi, lakini pia kwa Taifa kwa ujumla, ambapo watafanya biashara mbalimbali.

"Mradi utakapo kamilika utasaidia kuinua kipatao na kutupatia ajira kwenye bandari pamoja na kufanya biashara mbalimbali. Natamani hata mradi huu umalizike mwakani kwani ni mradi mkubwa na utatusaidia," amesema Hafidhi.

Kwa upande wake, Jamila Sabu, Mkazi wa Kilwa Masoko, anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea mradi huo wa bandari, na kwamba utawainua kiuchumi.

"Yaani kama mimi mama ntilie, nipo hapa nafanya biashara zangu za chakula, ni fursa mojawapo kwangu, kwa kuwa napata kipatao, hawa walioajiriwa humu kwenye ujenzi, wanakula kwangu; lazima nishukuru Serikali kwa jitihada za kuleta mradi huku," amesema Jamila.

Rais Samia anatarajia kuweka jiwe la msingi katika mradi huo wa bandari, sambamba na kugawa boti na nyavu kwa wavuvi wa Kilwa Masoko.