Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watano wafariki, 28 wajeruhiwa ajali ya basi la Shabiby, lori

Muktasari:

  • Ajali hiyo imehusisha basi la Kampuni ya Shabiby lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Dodoma baada ya kupinduka katika eneo la Tanangozi mkoani Iringa alfajiri ya leo Mei 8, 2026 na kusababisha vifo vya watu watano pamoja na majeruhi 28.

Iringa. Watu watano wamefariki dunia na wengine 28 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Shabiby aina ya Youtong likiendeshwa na Michael Mbugi likitokea Dodoma kwenda Mbeya na kupata ajali katika eneo la Tanangozi, Kata ya Mseke mkoani Iringa, alfajiri ya leo Mei 8, 2026 baada ya kugongana na lori la vinywaji aina ya FAU.

‎Akithibitisha taarifa hiyo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa, Dk Alfred Mwakalebela amesema hospitali hiyo imepokea majeruhi 28 waliotokana na ajali hiyo pamoja na miili ya watu watano waliofariki dunia.

‎Dk Mwakalebela amesema kati ya majeruhi hao, wanaume ni 16 wakiwemo watoto wanne, huku wanawake wakiwa 12.

‎Kwa mujibu wa daktari huyo, mmoja wa majeruhi mwenye asili ya Asia amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) kutokana na kuumia zaidi kichwani.

‎“Majeruhi wengine hali zao ni mbaya na wanaendelea kupatiwa matibabu. Wapo waliopata majeraha ya kichwa, mmoja jicho limetoka na kuna taratibu zinaendelea  huyo mmoja ambaye ameumia sana kumhamishia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi,” amesema Dk Mwakalebela.

Basi la Shabiby likiondolewa katika eneo la Tanangozi kata ya Mseke mkoani Iringa baada ya kupata ajali. Picha na Mtandao

‎Dk Mwakalebela ameongeza kuwa watu 11 waliopata majeraha madogo tayari wameruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu.

‎Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Iringa, DkMwakalebela amesema madaktari wanaendelea kutoa huduma kwa majeruhi wengine.

Mkuu wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari la lori kushindwa kushuka vizuri katika barabara hiyo eneo la Tanangozi ambapo kuna mteremko mkali.

‎"Chanzo cha ajali ni dereva wa lori aina ya FAU kushindwa kuendesha vizuri gari katika eneo la Tanangozi lenye mteremko mkali," amesema Kamanda Bukumbi.

‎Aidha Kamanda Bukumbi ametoa wito kwa madereva kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa vyombo vya moto kabla ya kuingia na wawapo barabarani ili kuepusha ajali.