Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili wafariki dunia, saba wajeruhiwa ajali basi na lori Korogwe Tanga

Ajali iliyohusisha magari mawili ikiwemo la basi na gari la mizigo katika Kijiji cha Bwiko Korogwe leo April 22,2026 na kusababisha vifo vya watu wawili na majeruhi saba. Picha na Mbonea Herman.

Muktasari:

  • Polisi imeeleza kuwa watu wawili wamefariki dunia na wengine saba wamejeruhiwa baada ya basi kugongana uso kwa uso na lori Korogwe, huku chanzo kikitajwa kuwa uzembe wa dereva wa basi.

Tanga. Watu wawili wamepoteza maisha kutokana na ajali ya basi la abiria na gari la mizigo kugongana uso kwa uso katika Kijiji cha Bwiko, Kata ya Mkomazi, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, kwenye barabara kuu ya Korogwe–Moshi.

Gari la abiria lililohusika katika ajali hiyo ni mali ya Kampuni ya Mapenzi ya Mungu, huku gari la mizigo ni Mitsubishi Fuso.

Ajali hiyo imetokea leo Jumatano, Aprili 22, 2026 saa kumi alfajiri, ambapo watu waliofariki ni dereva wa gari la mizigo na abiria mmoja wa basi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema gari la mizigo lilikuwa likitokea Moshi kuelekea Dar es Salaam, wakati basi la abiria lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Arusha.

Kamanda Mchunguzi amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi kushindwa kulimudu gari lake na kuhama kutoka upande wake wa kushoto wa barabara na kuingia upande wa kulia.

“Kutokana na hali hiyo, magari hayo yaligongana uso kwa uso na kusababisha watu wawili kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya,” amesema Mchunguzi.

Kuhusu miili ya marehemu, Mchunguzi amesema imehifadhiwa katika Kituo cha Afya cha Mombo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa daktari na taratibu nyingine zinazofuata, huku majeruhi saba, wote wakiwa abiria wa basi, wamepelekwa katika Kituo cha Afya cha Hedaru kwa ajili ya matibabu.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limetoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani, kuepuka uzembe na kudhibiti vyombo vyao wanapokuwa barabarani ili kuzuia ajali zinazoweza kuepukika.

“Watumiaji wote wa barabara wanakumbushwa kuwa usalama barabarani ni jukumu la kila mmoja,” amesema Kamanda Mchunguzi.