Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watano kizimbani wakidaiwa kuhujumu miundombinu SGR

Watuhumiwa wa uhujumu miundombinu ya reli ya kisasa (SGR) wakipelekwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kibaha. Picha na Sanjito Msafiri

Muktasari:

  • Wamo raia wa kigeni, wapelekwa rumande.

Kibaha. Watu watano wakiwemo raia wa kigeni wamefikishwa mahakamani mkoani Pwani wakikabiliwa na mashItaka ya kuhujumu miundombinu ya reli ya kisasa (SGR) na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh200 milioni.

Waliofikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kibaha leo Desemba 17, 2024 ni Zhang Feng, Wang Yong, Paulo John, Abdul Mohamed na Pius Kitulya, wakazi wa Miwaleni, Mlandizi, wilayani Kibaha.

Mwendesha mashitaka Wakili wa Serikali, Joseph Kisaka amedai mahakamani hapo kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Novemba  na Desemba, 2024.

Hakimu Felister Ng'welu anayesikiliza kesi hiyo amewataka washtakiwa kutojibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo.

Baada ya kusomewa mashitaka wamepelekwa rumande. Kesi imepangwa kutajwa Desemba 30, 2024.

Kesi hiyo imevuta watu wengi waliofika mahakamani kuisikiliza.

Licha ya kusikilizwa jioni, baadhi ya watu waliokuwa nje ya mahakama baada ya kesi kuitwa waliingia ndani kusikiliza.