Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanne kortini wakidaiwa kusafirisha kilo 23 za bangi

Washtakiwa wanaokabiliwa na mashtaka matatu ya kusafirisha bangi kilo 23 na gramu 542.6 wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu, baada kusomewa mashtaka yao. Picha na Hadija Jumanne.

Muktasari:

  • Washtakiwa hao akiwemo mwanamke mjamzito, wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kusafirisha bangi, tukio wanalodaiwa kulitenda, Oktoba 19 na Oktoba 20, 2023 eneo la Mbondole Msongola.

Dar es Salaam. Watu wanne akiwemo mwanamke mjamzito, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka matatu ya kusafirisha bangi kilo 23 na gramu 542.

 Washtakiwa hao ni Hassan Magoha (48) mkazi wa Somangila; Husein Shaban (32); Tarik Husein (23) na Zainabu Athuman (24) wote wakazi wa Mbondole Msongola, Wilaya ya Ilala.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo, leo Novemba 14, 2023 na kusomewa mashtaka yao wakili wa Serikali, Winiwa Samson akishirikiana na John Kaombwe, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Evodia Kyaruzi.

Akiwasomewa mashtaka yao, Wakili Samson alidai shtaka la kwanza, lina mkabili mshtakiwa kwa kwanza na wa pili katika kesi hiyo, ambapo wanadaiwa Oktoba 19, 2023 eneo la Somangila lililopo Kinondoni, washtakiwa kwa pamoja walikutwa wanafirisha bangi zenye uzito wa kilo 1.89.

Shtaka la pili, linawahusu washtakiwa wote ambapo wanadaiwa Oktoba 20, 2023 eneo la Mbondole, Wilaya ya Kigamboni, walikutwa wakisafirisha bangi yenye uzito wa kilo 21.89, kinyume cha sheria.

Shtaka la tatu linahusu mshtakiwa wa kwanza, wapili na wanne, ambao wanadaiwa Oktoba 20, 2023 eneo la Mbondole, Wilaya ya Kigamboni, walikutwa wakisafirisha bangi yenye uzito wa gramu 542.6 kinyume cha sheria.

Washtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili, wamekana kutenda makosa hayo.

Upande wa mashtaka ilidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mkyaruzi alisema washtakiwa hanawa dhamana kwa kuwa kiasi cha bangi walichokutwa nacho ni kikubwa na kinazidi kilo 20.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Kyaruzi aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 28, 2023 itakapotajwa.

Washtakiwa watarudishwa rumande kutoka na kiasi cha dawa wanazodaiwa kusafirisha kuvuka kilo 20.