Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanasayansi Afrika kujadili utafiti wenye tija

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Bodi ya Wanasayansi wa Kiafrika (Afrique One-Reach) wakifuatulia mkutano huo unaojadili masuala mbalimbali ya tafiti  zitakazosaidia kupunguza changamoto zinazokabili nchi mbalimbali za Afrika, leo Februari mosi, 2024 jijini Arusha.Picha na Janeth Mushi

Muktasari:

  • Wanasayansi hao wanakutana kupitia Bodi ya Afrique One Reach, kujadili jinsi ya kufanya utafiti utakaosaidia kupunguza changamoto zikazokabili jamii yakiwemo magonjwa ya milipuko, magonjwa yasiyopewa kipaumbele na yale yasiyoambukiza.

Arusha. Bodi ya Wanasayansi wa Afrika (Afrique One Reach) inakutana jijini Arusha kujengeana uwezo wa kufanya utafiti wenye tija wa kukabiliana na uharibifu wa mazingira, magonjwa ya kuambukiza, yasiyoambukiza na yasiyopewa kipaumbele.

 Akizungumza leo Alhamisi, Februari mosi, 2024 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa bodi hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa programu hiyo, Sayuki Mfinanga amesema wamelenga kujenga uwezo wa afya kupitia wanafunzi na kuja na suluhisho.

“Wanafunzi wetu tumewapangilia kwanza wameandika na kuja na mawazo yao ya kitafiti kwa sababu katika ngazi za shahada za uzamili na shahada za uzamivu tunawafundisha kuwa watafiti kuwa wabobevu katika maneo hayo,” amesema.

Mfinanga amesema wamewagawa wanafunzi hao katika makundi ya utafiti wa magonjwa yasiyoambukiza, magonjwa yanayotoka kwa wanyama na kuja kwa binadamu, magonjwa yasiyopewa kipaumbele, wakitegemea kuja na suluhisho.

 “Tunataka tujenge uwezo na utafiti utakazosaidia kushughulika na watu ili wabadilishe tabia tupate watu wenye afya nzuri na tutajenga uchumi wa nchi na Afrika kwa ujumla,” amefafanua.

Mkurugenzi wa Afrique One-Reach, Profesa Bassirou Bonfoh amesema wataalamu hao kutoka sekta mbalimbali watajengewa uwezo wa kufanya utafiti kusaidia Serikali za nchi za Afrika.

Amesema kupitia programu hiyo ya awamu ya tatu, vijana 61 watanufaika na mafunzo ya kufanya utafiti.

Profesa huyo amesema lengo la programu ni kuzalisha maarifa ya mabadiliko ya udhibiti wa magonjwa ikiwemo yasiyopewa kipaumbele, kujenga mikakati ya kuangalia mipango ya kitaifa ya afya na jamii.

Amesema kupitia mkutano huo wa siku saba, watapitia mada, kujadiliana, kubadilishana uzoefu na kukuza ushirikiano katika nchi za Afrika ili kufanya tafiti zenye mafanikio.

“Tangu mwaka 2009 tumeandaa programu hii na hii ni awamu ya tatu, kwani tunaamini katika kufanya tafiti katika afya moja juu ya magonjwa mbalimbali ikiwemo yanayotoka kwa wanyama na kuja kwa binadamu, ili tuje na majibu ya changamoto zinazokabili jamii hasa magonjwa ya milipuko,” amesema.

Naye Mtafiti Mwandamizi na Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti cha Kilimanjaro Clinical Research Institute, Profesa Blandina Mbaga amesema mkutano huo unalenga kujenga uwezo kwa watafiti, ili kupambana na matatizo yanayosababishwa na mwingiliano wa mazingira na hali ya hewa kwa ujumla.

“Tangu mpango umeanza kwa ujumla ni wanafunzi wengi wamefundishwa na machapicho mengi, sera nyingi zimechangiwa za kitaifa na kimataifa kutokana na ugunduzi wa utafiti huo.

“Awali tulianza na sekta ya wanayama, ila awamu ya pili tukachanganya sekta ya wanyama na binadamu baada ya kuanza dhima ya afya moja, tukaunganisha zote,” amesema.