Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi wamuweka kitimoto Waziri Ummy

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu (katikati) akizungumza.

Muktasari:

  • Wakazi wa Kata ya Mbagala, wamempa changamoto Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, baada ya kulalalmikia ufinyu wa eneo la Hospitali ya Mbagala Rangitatu, idadi ndogo ya wataalamu kulinganisha na wagonjwa na hivyo kusababisha msongamano wa wagonjwa.

Dar es Salaam. Katika hali isiyo ya kawaida, wananchi waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Mbagala Rangitatu wamempokea Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwa malalamiko makubwa mawili yaliyojikita katika ufinyu wa eneo na matibabu bure kwa makundi maalum.

 Wananchi hao wamesema hospitali hiyo kwa sasa imezidiwa na kwamba ujenzi wa jengo la ghorofa sita uharakishwe kwani wanatumia muda mrefu wawapo hospitalini hapo, huku wakimbana zaidi kuhusu matibabu bure kwa makundi maalum.

Waziri Ummy amekutana na malalamiko hayo leo Jumatano, Agosti 9, 2023 hosipitalini hapo, wakati akiendelea na ziara yake ya kutatua changamoto ya ufinyu wa maeneo, unaozikabili hospitali na vituo vya afya mkoani Dar es Salaam.

Kufuatia malalamiko hayo, Waziri Ummy, amesema kwa sasa hospitali hiyo inapanuliwa kwa kuongezwa jengo la ghorofa sita; lenye thamani ya Sh10.8 bilioni, litakalowezesha kupunguza msongamano huo.

Amesema Serikali imetoa ekari 30 eneo la Vikuruti itakayojengwa hospitali mbadala wa Mbagala ili kuondoa changamoto hiyo na kwamba zahanati mbili jimbo la Temeke zitapandishwa hadhi na kuwa vituo vya afya.

"Mbagala ni eneo finyu, nimeagiza kuharakishwa kwa jengo hili ili huduma zianze na huduma bora za afya ziendelee na Mwenyekiti wa Halmashauri nadhani mtaendesha ujenzi huu ukamilike kwa wakati kwani Serikali itakamikisha fedha kwa wakati," amesema na kuongeza;

"Tunatambua watumishi wa afya wa Mbagala ni wachache na wagonjwa ni wengi mno hapa, naomba fanyeni kwa moyo na zingatieni weledi mnapotoa huduma ili iwe bora na salama, tutoe huduma kwa kuzingatia viapo vyenu, upendo na utu."

Wananchi hao wametaka msamaha wa makundi maalum uongezewe wigo mpana kwani wengi wamekuwa wakitozwa fedha katika baadhi ya huduma.

"Msongamano hapa ni mkubwa sana, tunashauri vyumba viongezwe maana tunakuja tangu asubuhi saa tatu tupo hapa, sasa ni saa 6 mchana na hatujamuona daktari, watu ni wengi na vyumba vya madaktari ni vichache tunaomba viongezwe," amesema Tabu Hassan mkazi wa Kongowe.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya Mbagala Rangitatu, Dk Ally Mussa amesema wanakabiliana na changamoto ya ufinyu wa eneo na miundombinu pamoja na watumishi wachache licha ya kwamba wanahudumia wagonjwa wengi.

"Kinamama 40 wanajifungua kwa siku, tunafanya oparesheni 7 mpaka 12 kwa siku. Hali ya msamahama tunatoa Sh22 milioni kila mwezi kulingana na sera ya watoto chini ya miaka mitano, wajawazito na wazee wasiojiweza zaidi ya miaka 60….” Amesema Dk Mussa.