Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanajeshi 88 washindwa kumaliza kozi TMA

Muktasari:

  • Maofisa wanafunzi 575 wamevishwa vyeo vya Luteni Usu baada ya kuhitimu mafunzo Chuo Cha Kijeshi Monduli huku wenzao 88 washindwa kumaliza mafunzo hayo ambapo 14 wayakimbia.

Monduli. Wanafunzi 88 waliojiunga na Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) mkoani Arusha, wameshindwa kumaliza mafunzo kwa sababu mbalimbali ambapo kati yao, 14 wadaiwa kuyakimbia ambapo mhitimu hutunukiwa “Shahada ya Sayansi ya Kijeshi.”

Imeelezwa kuwa chuo hicho cha mafunzo ya kijeshi, kwa kushirikiana na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), wamekuwa wakitunuku shahada hiyo kwa wanafunzi hao, ambayo kimsingi inawaandaa maofisa waliohitimu kuweza kuwa mahiri katika kusimamia masuala ya kijeshi, amani pamoja na uongozi kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Hayo yamebainishwa katika mahafali ya leo Jumamosi Novemba 18, 2023 ambapo maofisa wanafunzi 575, wametunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu, Rais Samia Suluhu Hassan na hivyo kuvishwa vyeo vya Luteni Usu.

Akitoa taarifa ya mafunzo hayo, Mkuu wa chuo hicho, Brigedia Jenerali Jackson Mwaseba amesema kulikuwa na makundi mawili wa wanafunzi ambapo katika kundi la 04/20 la maafisa wa wanafunzi wa shahada ya Sayansi ya Kijeshi, waliojiunga na chuo walikuwa 73 huku 62 ndiyo walifanikiwa kuhitimu.

Amesema wanafunzi 11 walishindwa kumaliza mafunzo hayo kutokana na sababu kadhaa ikiwepo ugonjwa, kitaaluma, uaminifu, tabia na nidhamu.

Kwa upande wa kundi la 70/22; wanafunzi 77 kati ya 524 waliojiunga na mafunzo wameshindwa ambapo kati yao 14 walikimbia.

Brigedia Jenerali Mwaseba ameweka wazi sababu na namba ya wanafunzi ambao wameshindwa kumaliza mafunzo kuwa ni pamoja na kukosa uaminifu (wanafunzi 15), ugonjwa (19), makosa ya tabia (3), taaluma (22) na huku kwenye uadilifu wakiwa ni wanafunzi wanne.

Amesema Wanafunzi 66 walitoka Makao Makuu ya Jeshi na walikuwa katika mafunzo mbalimbali nje ya nchi wakiwepo marubani wanane.