Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafunzi watatu Udom wafariki ajali ya gari

Muktasari:

Wanafunzi watatu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea jana jioni katika moja ya barabara zilizopo chuoni hapo.

Dodoma. Wanafunzi watatu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) wamefariki dunia na wengine watano wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea jana jioni katika moja ya barabara zilizopo chuoni hapo.

 Akizungumza leo Jumapili Juni 5, 2022 na Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Beatrece Baltazar amesema ajali hiyo imetokea jana saa 2.00 usiku.

Amewataja waliofariki kuwa ni Hana Meshack, Zira Mpenda, Mpeli Mahenge.

Beatrece amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Fortunata Kingazi, Fibi Julius, Sifa Shora, Enica William na mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Furahina.

Amesema majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa na hali zao zinaendelea vizuri.

Taarifa zinasema wanafunzi hao walikuwa wanatoka katika mahafali ya dini yaliyokuwa yakifanyika chuoni hapo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Martin Otieno ameahidi kutoa taarifa baadaye.