Waliotarajia kuvuna mbegu ya sungura watapeliwa

picha ya sungura kwa hisani ya mtandao wa kijamii
Muktasari:
Wafugaji hao walieleza kuwa walipanda mbegu za sungura katika mradi wa ufugaji kibiashara, unaoendeshwa na Kampuni ya The Rabbit Bliss Limited yenye ofisi zake Ngaramtoni nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Arusha. Zaidi ya wafugaji 20 wa sungura mkoani Arusha, wanadaiwa kutapeliwa mamilioni ya fedha baada ya ‘kupanda mbegu ya sungura’ lengo likiwa ni kuvuna siku za baadaye.
Wafugaji hao walieleza kuwa walipanda mbegu za sungura katika mradi wa ufugaji kibiashara, unaoendeshwa na Kampuni ya The Rabbit Bliss Limited yenye ofisi zake Ngaramtoni nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika ofisi za gazeti hili juzi, wakulima hao walisema walijiunga na kampuni hiyo mwaka jana kwa malengo ya kupanda mbegu ya sungura lakini wamejikuta wakiingizwa mjini.
Mmoja wa wakazi hao, Godson Makundi alisema alijiunga na kununua majike matano ya sungura na dume moja kwa Sh950,000.
Makundi alieleza kwamba baada ya muda alizalisha sungura 21 na kuwapeleka kwenye kampuni hiyo kuwauza, lakini hadi sasa hajalipwa.
Akijibu tuhuma hizo kwa simu, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Payas Ruben alisema wamefanya mabadiliko ya uongozi ambayo yamechangia hali hiyo.
Habari zaidi soma Gazeti la Mwananchi