Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wagonjwa sita kupandikizwa figo Muhimbili


Muktasari:

  • Hospitali ya Muhimbili imeshapandikiza figo watu 75 hadi sasa.

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), inatarajia kufanya upandikizaji figo kwa wagonjwa sita ifikapo Julai.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Juni 30, 2023 na Mkuu wa Kitengo cha Figo Muhimbili, Dk Jonathan Mngumi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo.

Dk Mngumi ambaye ni daktari bingwa magonjwa ya figo amesema hadi sasa, wameshapandikiza figo watu 75.

“Tumejadili na Mkurugenzi Mtendaji, tunatarajia Julai tutafanya tena huo upandikizaji na tuna wagonjwa sita wanaosubiri huduma hiyo,” amesema.

Aidha Dk Mngumi amesema idadi ya watu wenye uhitaji wa huduma kuchuja ya kusafisha damu kwa njia ya mashine imeongezeka ambapo amesema, dunia wagonjwa ni milioni 800, sawa na asilimia 10 ya idadi wa wote wana magonjwa ya figo.

Tanzania ina asilimia saba ya watu wanaotambuliwa kuwa na magonjwa sugu ya figo na wanaongezeka kwani katika kliniki yao ya wagonjwa wa figo kwa wiki hupokea wastani wa watu 90 wanaopima figo zao na watano kati yao hutakiwa kuanzishiwa huduma ya kuchuja damu kwa kutumia mashine kitaalamu ikijulikana Dialysis.

“Mtu mmoja hutakiwa kuchuja damu kwa saa nne kwa siku na anatakiwa kufanya hivyo mara tatu au mbili kwa wiki. Ni huduma yenye gharama kubwa kwa wagonjwa na inabebesha mzigo mkubwa kwa taasisi na Serikali kwa ujumla,” amesema Dk Mngumi.

Naye Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Mohammed Janabi amesema kwa siku hospitali hiyo huchuja damu wagonjwa 130 hadi 150.

Miongoni mwa wagonjwa hao, wagonjwa 30 hadi 50 hupata huduma katika hospitali ya Mloganzila.

Profesa Janabi ametoa rai kwa watu kutunza afya zao kwani huduma ya kuchuja figo ni gharama na vifaa na dawa zinazotumika, zinatoka nje ya nchi na asilimia 30 hadi 40 ya wagonjwa wanaohitaji hawana uwezo wa kumudu.

Hata hivyo amesema zaidi ya asilimia 90 ya wagonjwa hao ambao huchuja damu ambayo amesema siyo siyo tiba ya mwisho, kwani wengi wao wanasubiria kupandikizwa figo kama tiba kamili.

“Kuna wale wenye bima ya afya na wengine wachache wanaotoa fedha zao mfukoni hata wao hawana uhakika watatoa kwa muda gani,” amesema.

Pia amesema katika wagonjwa 100, kati yao 90 wana shinikizo la juu la damu, na hivyo ametoa rai kwa Watanzania kujikinga ikiwamo kupunguza matumizi ya chumvi mezani.