Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafanyabiashara waagizaji mizigo kunufaika huduma ya bima kidigitali

Muktasari:

  • Waingizaji wa mizigo wadogo, wa kati nchini kuanza kunufaika na huduma mpya ya kidijitali ya bima ya mzigo itakayotolewa kupitia simu za mkononi kuwawezesha kusafirisha mizigo yao kutoka nje nchi kuja nchini

Dar es Salaam. Katika jitihada za kuboresha maisha ya watanzania kupitia mtandao wa kidijitali, Kampuni ya mawasiliano ya Tigo, imezindua bima ya mizigo kupitia simu itakayowasaidia iwatumiaji kupata njia rahisi ya kusafirisha mizigo yao kutoka nje ya nchi.

Kupitia teknolojia hiyo itawanufaisha waingizaji wa mizigo wadogo, wa kati kutoka nje kwa njia za barabara, angani, au baharini.

Huduma hiyo ya kimapinduzi nchini ilizinduliwa Julai11, 2024 na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Kampuni za Sanlam Insurance, Smart Policy, na Busara Insurance Broker na itawawezesha wateja wake wateja wa mtandao huo kunufaika.

Akizungumzia mapinduzi hayo, Ofisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha amesema kama waasisi wa mazingira ya maisha ya kidijitali nchini wanatafuta ushirikiano unaleta thamani kwa huduma wanzotoa.

“Dhamira yetu ni kutoa suluhisho za malipo ya haraka na rahisi kwa mizigo ya wateja wetu. Ushirikiano huu wa kimkakati unatumia nguvu za pamoja za pande zote zilizohusika na kuweka msingi wa uwezo mzuri wa bima na uwekezaji wa kidijitali kote nchini," amesema.

Pesha amesema ubunifu huo wa kimtandao unazingatia usalama kwa mizigo yao ya nje, kulingana na mahitaji ya lazima ya bima kwa bidhaa zote zinazoingia.

“Bima ya Mizigo siyo tu kwamba inabadilisha upatikanaji wa bima kwa watumiaji wa Tigo Pesa, pia inarahisisha mchakato kwa upatikanaji rahisi kupitia simu. Mpango huu unarahisisha safari ya mteja na kuashiria enzi mpya ya urahisi na usalama,” amesema Pesha.

Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa Sanlam General Insurance, Geofrey Masige alisema wanajivunia ushirikiano huo wa kuleta kuleta utaalamu na uaminifu wao katika suluhisho hilo la kimapinduzi la bima ya mizigo.

“Tunaelewa umuhimu wa kulinda bidhaa zinazoingizwa dhidi ya hatari na hali zisizotarajiwa. Ushirikiano huu unasisitiza dhamira yetu ya kutoa bidhaa za bima za kina na za ubunifu zinazokidhi mahitaji yanayobadilika ya biashara nchini."

Mratibu wa Miradi kutoka SmartPolicy, Farheen Ghartey, alisema wataendelea kutumia majukwaa ili kuwezesha uuzaji wa bidhaa za bima zinazokidhi mahitaji yanayobadilika ya soko.

“Kuhakikisha upatikanaji na ufanisi katika miamala ya bima; na kwa ushirikiano huuu tunawawezesha wafanyabiashara nchini Tanzania kupata na kununua bima ya mizigo kwa urahisi kupitia mchakato wa kidijitali," amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Busara Insurance Brokers, James Samson alisema ushirikiano huo utasaidia kupenya kwa sera muhimu za ulinzi wa biashara.

“Bima ya mizigo ya nje inalinda mizigo ya thamani kutoka bandari ya kuondoka hadi kufika Tanzania. Bidhaa hii inatoa njia kwa waingizaji wa mizigo wadogo, wa kati, na wakubwa kupata bima kwa urahisi na pia bidhaa hii imeundwa na mchakato rahisi wa malipo ya madai," amesema.

Wateja wa Tigo Pesa wanaweza kupata huduma ya Bima ya Mizigo kwa kupiga 15001#, kisha chagua Huduma za Kifedha (7), chagua Bima (3) na chagua Bima ya Mizigo (4) na fuata hatua rahisi kukamilisha mchakato.