Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafanyabiashara Iringa wafungua maduka, wananchi wapata ahueni

Muktasari:

  • Mwananchi Digital imeshuhudia wafanyabiashara mkoani Iringa wakiendelea kufungua maduka kuanzia saa nane mchana huu.

‎Iringa. Baada ya saa kadhaa za sintofahamu, hatimaye wafanyabiashara katika Mkoa wa Iringa wamefungua maduka yao na wananchi wameanza kupata huduma za manunuzi ya bidhaa mbalimbali, hatua inayowapa ahueni.

‎Akizungumza na Mwananchi Digital Leo Mei 12, 2025, Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Iringa, Benito Mtende amesema kuwa wamefanikiwa kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba katika kikao cha ndani walichokifanyia ofisini kwa kiongozi huyo.

‎Maduka hayo yameanza kufunguliwa kuanzia saa nane mchana na kuendelea.

‎"Tumekutana na mkuu wa mkoa ofisini kwake, tumeeleza changamoto zetu na ametuahidi kuwa mambo yote yaliyofikishwa mezani kwake yatashughulikiwa kwa haraka," amesema Mtende.

‎Mtende ameongeza kuwa kikao hicho kilikuwa cha mafanikio kwa pande zote na kilitoa matumaini kwa wafanyabiashara waliokuwa wamefunga maduka yao kama njia ya kuwasilisha kilio chao.

‎"Wafanyabiashara wameonyesha mshikamano mkubwa na sasa wanarudi kazini wakiwa na matumaini kuwa sauti zao zimesikika," amesisitiza Katibu Mtende.

"Nimefurahi kurudi kazini. Tumevumilia sana, lakini sasa tuna imani kuwa Serikali inatusikiliza," amesema Rehema Mbise, mfanyabiashara wa nguo mkoani Iringa.

‎ Ally Mussa, ambaye ni muuzaji wa vifaa vya simu, naye ameeleza kwamba kutokana na kikao walichohudhuria viongozi wao kuonekana kuwa na majibu chanya wameamua kufungua maduka.

‎"Wateja wangu wengi walikuwa wakinipigia simu wakiulizia huduma na baada ya kufungua duka wamekuja kwa wingi na hii ni dalili kuwa wananchi walikuwa wakisubiri huduma," amesema Ally na kuongeza kuwa,

‎"Tulikuwa tumekata tamaa, lakini kwa sasa tunaona mwanga. Tutarudi kwa nguvu mpya."  ‎

‎"Asubuhi ya leo nilihangaika sana kupata sabuni. ila sasa hivi nimeipata kirahisi," amesema Mwanaidi Kipanga, mkazi wa Kihesa.

‎Vilevile Katibu Mtende ametoa rai kwa wanachama wa jumuiya hiyo kuendelea kuwa wavumilivu huku wakisubiri utekelezaji wa ahadi uliotolewa na viongozi wa mkoa.