Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waendesha bodaboda 3,032 wasajiliwa

Muktasari:

  • Naibu Waziri amesema waendesha pikipiki hao walikuwa wamesajiliwa kwenye mfumo wa utambuzi, usajili na utoaji wa vitambulisho vya kidijitali na mpango huo unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Dodoma. Hadi kufikia Mei 11, 2025 waendesha bodaboda 3,032 walikuwa wamesajiliwa kwenye mfumo wa utambuzi, usajili na utoaji wa vitambulisho vya kidijitali, Bunge limeelezwa.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake Jinsia na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis leo Alhamisi Mei 15, 2025 ambapo amesema Serikali inao mkakati wa kuwatambua na kuwasajili wafanyabiashara ndogondogo nchini wakiwemo waendesha bodaboda.

Mwanaidi alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Asha Abdullah Juma aliyeuliza lini Serikali itaanzisha utaratibu wa kuwasajili waendesha bodaboda nchini.

Mbunge huyo ameuliza ni kwa nini jambo hilo linakuwa la hiyari badala ya kulifanya kuwa la lazima ili kuwasaidia waendeshaji wa bodaboda wawe kwenye mfumo mzuri na kutambulika.

Naibu Waziri amesema waendesha pikipiki hao 3,032 ambao wanaume ni 2,921 na wanawake 111 walikuwa wamesajiliwa kwenye mfumo wa utambuzi, usajili na utoaji wa vitambulisho vya kidijitali na mpango huo unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

“Usajili huo ni wa hiari na umeanza Machi 2024 na unatekelezwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tamisemi kupitia Dawati la Uratibu wa Wafanyabiashara Ndogondogo ambalo limeanzishwa katika mamlaka za serikali za mitaa zote 184 nchini,” amesema Mwanaidi.

Hivyo, shughuli hiyo ya usajili inaendelea kwa kushirikiana na maofisa waliopata mafunzo katika mamlaka za serikali za mitaa nchini kote na linatarajia kuendeshwa katika mazingira rafiki.

Kuhusu usajili wa lazima kwa waendesha pikipiki, Naibu Waziri amesema hakuna uhiyari kwani wanasajiliwa kwa lazima katika uendeshaji wa vyombo vyao isipokuwa usajili unaozungumziwa ni kwa ajili ya kuwawezesha waendesha bodaboda kujipatia kipato katika biashara.