Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau wataka elimu iakisi maarifa

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Miyuji wakiwa kwenye kikao cha kuutambulisha mradi wa HEET utakaotekelezwa na Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP)

Muktasari:

  • Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) kimepata Sh6.85 billioni kwa ajili ya kuendeshea mradi wa elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET).

Dodoma. Wakazi wa Kata ya Miyuji jijini hapa wametaka fedha zilizotolewa na Serikali kuboresha miundombinu ya Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP), zionyeshe matunda kwa wahitimu kutumia maarifa waliyoyapata kwenye jamii.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Oktoba 5, 2023 na Ofisa Elimu Kata ya Miyuji, Grace Risasi kwenye kikao cha wadau wanaozunguka chuo hicho kilichokuwa na lengo la kuutambulisha mradi wa HEET utakaotekelezwa kwa miaka mitano.

Risasi amesema wao kama jamii wamekuwa wakiwaona vijana waliomaliza vyuo wakihangaika na bahasha mikononi kwa ajili ya kutafuta kazi lakini linapokuja suala la kupata ajira hizo wanakuwa hawana uwezo wa kufanyia kazi maarifa waliyopata.

Amesema mradi huo uwe chachu ya kuwatengeneza vijana wanaomaliza chuoni hapo kuwa na ushindani kwenye soko la ajira.

Akitambulisha mradi huo kwa viongozi wa Serikali za mitaa na jamii inayozunguka chuo hicho, Mratibu wa mradi huo, Said Panga amesema lengo mojawapo la mradi huo ni kutoa elimu inayoendana na soko ili wahitimu waweze kujiajiri au kuajirika.

Amesema lengo lingine ni kuboresha miundombinu ya chuo hicho ili iwe rafiki kwa wanachuo wote hata wale wenye mahitaji maalum kwa kutoa elimu bora kupitia mitaala ambayo itawafanya wawe na ushindani kwenye soko la ajira.

"Lengo la mradi huu kama unavyojieleza ni kuboresha mageuzi ya kiuchumi hivyo vijana watakaopitia chuo hiki watakuwa na uwezo wa kujitegemea kiuchumi tofauti na ilivyokuwa hapo awali," amesema Panga

Amesema pia ili kutoa elimu bora kwa kila mwanachuo watatumia teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) ili kuwawezesha kusoma na kuuliza maswali wakiwa nyumbani au ofisini na hivypo kutolazimika kufika chuoni.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho, Profesa Hozen Mayaya, ameitaka jamii inayozunguka chuo hicho kutumia fursa ya uwepo wa chuo kiuchumi, kwani wanafunzi 10,000 na watumishi 418, wanategemea kupata huduma za mahitaji mbalimbali kutoka kwa wakazi wa kata hiyo.

Pia amesema uwepo wa chuo hicho unalemeta fursa mbalimbali has katika sekta ya nyumba na makazi, saluni za kike na za kiume, usafiri na biashara za maduka.

Aidha amesema Sh6.85 billion zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya mradi wa HEET zinaweza kuonekana kuwa ni chache kutokana na mahitaji ya chuo lakini serikali imeendelea kuwekeza fedha nyingi chuoni hapo kwa ajili ya kuhakikisha mazingira ya kufundisha na ujifunzaji yanakuwa mazuri.