Wabunge Afrika Mashariki waipa ushauri Tanzania

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashiriki (EAL),Makongoro Nyerere.
Muktasari:
Wakizungumza baada ya kufanya ziara hiyo walisema ipo haja kwa Tanga kutangaza vivutio vingine.
Mkinga. Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Eala) wametembelea mpaka wa Horohoro uliopo kati ya Tanzania na Kenya na kuitaka Serikali kutumia fursa ya ujio wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga kuweka vivutio kwa wawekezaji.
Wakizungumza baada ya kufanya ziara hiyo walisema ipo haja kwa Tanga kutangaza vivutio vingine.
Mwenyekiti wa wabunge wa Eala kutoka Tanzania, Makongoro Nyerere amesema lengo la ziara hiyo ni kuona utekelezaji wa mpango huo utakavyowanufaisha wananchi wa jumuiya hiyo.
Naye Mbunge kutoka Tanzania, Adam Kimbisa ameishauri Serikali ya Mkoa wa Tanga kuandaa machapisho yenye kuainisha maeneo ya uwekezaji.
“Hii itasaidia wawekezaji kutambua vivutio vilivyopo,” amesema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela ameahidi kufanyia kazi maelekezo ya wabunge hao, akisema maandalizi yameanza kufanyika katika kuupokea mradi wa bomba hilo na kutangaza fursa za kiuchumi zilizopo.