Vimbunga vyenye majina ya kike ni balaa kuliko vya kiume

Mafuriko yakiwa yamezunguka makazi huku watu wakipanda juu ya majengo katika mojawapo wa miji nchini Msumbiji baada ya Kimbunga Idai kuikumbuka nchi hiyo mwezi uliopita. Picha na maktaba
Muktasari:
- Kwa mujibu wa Shirika la Hali ya Hewa la Duniani (World Meteorological Organisation), kuna orodha ya majina inayozunguka kulingana na vimbunga.
Dar es Salaam. Alikuja wa kwanza, kisha kaka yake. Katika kupepesa macho, vimbunga Idai na Kenneth vilibwaga mioyo na kuponya majeraha ambayo yangechukua miongo mingi kuponywa.
Mmoja baada ya mwingine, ndugu hao walijikuta wakiathiri maelfu ya kilomita katika nchi kadhaa walikosababisha uharibifu wa miundombinu na hasara nyinginezo kwa binadamu.
Kabla ya vimbunga hivyo kutokea, miaka 19 iliyopita kulikuwa na tarehe isiyosahaulika ya Eline. Hicho ni kimbunga kilichokuwa cha kitropiki ambacho kilidumu kwa siku tatu mfululizo.
Kama vile kilikuwa kikijua kinachofanya, kilishindilia ardhi, kung’oa na kuhamisha miamba na mawe makubwa.
Vilevile, kwa umbali mrefu kabisa tumesoma na kusikia kuhusu Dineo na Desmond na binamu, vimbunga vyenye ukorofi Wilma na Maria.
Idadi ni ndefu, ni ndugu wa familia iliyotawanyika ambayo kiulimwengu, wamegawanyika wakiwa na tabia ya uharibifu.
Mara chache tu, kama siyo zote, matukio haya mapya yameibuka katika nchi za Afrika Mashariki zikitembelewa na vimbunga Idai na Kenneth mwezi huu ambavyo vimeacha maswali mengi kuliko majibu.
Katika mitandao ya kijamii, Watanzania wenye mshangao wamekuwa wakitaka kujua baada ya kusalimika na kimbunga cha kitropiki cha Kenneth, Ijumaa iliyopita kililenga kufanya nini.
Lakini kwa nini matukio haya ya hali ya hewa yanapewa majina? Nani anayeamua yapewe majina?
Swali kama hilo limezuka baada ya ujio wa vimbunga katika msimu mmoja.
Inasemekana mtindo huu wa kuita majina vimbunga vya kitropiki ulianza miaka mingi iliyopita. Ilikuwa ni kwa lengo la kubainisha taarifa za athari za vimbunga. Majina yanatajwa kuwa njia rahisi ya kukumbuka kuliko namba na mambo ya kiufundi.
Kwa mujibu wa Shirika la Hali ya Hewa la Duniani (World Meteorological Organisation), kuna orodha ya majina inayozunguka kulingana na vimbunga.
Hata hivyo, siyo kila kimbunga kinakuwa kikubwa kiasi cha kupewa jina, ila vile tu vinavyotarajiwa kusababisha hasara kubwa.
Kwa mfano, nchini Uingereza kimbunga kinapewa jina kama kitakuwa na nguvu ya kusababisha madhara kwa rangi, kama njano- jitayarishe, nyekundu – chukua hatua, tahadhari.
Ajabu, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), vimbunga vyenye majina ya kike vinatajwa kuwa na madhara makubwa kwa binadamu kuliko vyenye majina ya kiume. Wanasayansi wanasema watu wanafikiri majina ya kike hayatishi sana, inaripoti BBC.
Kwa namna yoyote, inatarajiwa kuwa kutoa majina kwa vimbunga kunawafanya watu kuchukua tahadhari na kufikiria hatari ya vimbunga hivyo.
Mamlaka za hali ya hewa duniani zinaona inakuwa rahisi kufuatilia maendeleo ya vimbunga kwenye televisheni au mitandao ya jamii kama kukiwa na jina.
Kwa ujumla, inaaminika kuwa kukipa jina kimbunga ni kuvumisha tahadhari na kuipa nafasi jamii kujitayarisha.