Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana wajasiriamali watakiwa kuchangamkia fursa soko huru Afrika

Muktasari:

  • Akizungumza na vijana kutoka halmashauri saba za mkoa wa Arusha, Ofisa Biashara Mwandamizi kutoka wizara hiyo Festo Kapela,amesema kuna fursa nyingi katika soko huru la Afrika ikiwemo  kwa vijana wajasiriamali katika sekta ya kilimo hivyo wachangamkie fursa hizo kukuza kipato.

Arusha. Wizara ya Viwanda na Biashara,imewataka vijana wajasiriamali katika sekta ya kilimo ikiwemo wasindikaji wa mazao mbalimbali kuchangamkia fursa katika soko huru la Afrika.

Aidha wametakiwa kuhakikisha wanapozalisha mazao mbalimbali na uchakataji wa bidhaa,wazingatie sheria na kanuni ili ziweze kukidhi mahitaji ya soko ikiwemo usalama wa chakula.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Machi 21, 2025 na Ofisa Biashara Mwandamizi kutoka wizara hiyo Festo Kapela,akizungumza na vijana 60 kutoka halmashauri saba za mkoa wa Arusha,waliopatiwa mafunzo kupitia program ya Youth Entrepreneurship for the  Future of Food and Agriculture (Yeffa).

Festo ambaye pia ni Mratibu wa dawati la chakula na lishe, amesema vijana hao wakitumia elimu wanayoipata kupitia mradi huo wataweza kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika soko huru la Afrika ambalo linahitaji bidhaa zenye ubora.

“Tuko hapa kusisitiza katika eneo la kuongeza thamani mazo,vijana wengi mmeingia kwenye biashara,ni muhimu kutumia mafunzo haya kuboresha bidhaa na mazao mnayozalisha ili zikidhi mahitaji ya soko,kuna soko huru la Afrika linahitaji bidhaa zenye ubora,”amesema

“Tunawaelimisha juu ya uongezaji virutubishi kwenye mazao,mfuate kanuni na sheria pamoja na matumizi ya teknolojia,tutawasaidia kwa kushirikiana na wadau wengine ili kufikia ubora kwenye uzalishaji wa bidhaa zenu,muweze kushindana katika masoko ya ndani nay a kimataifa,”amesema

Kuhusu usalama wa chakula,amesema ni suala muhimu hasa katika kulinda afya ya mlaji na kufikia matakwa ya kisheria, kuanzia mnyonyoro mzima wa uzalishaji wa chakula lazima usaama wa chakula lipewe kipaumbele,”amesema Ofisa huyo

Awali Meneja anayesimamia urutubishaji wa vyakula viwandani kutoka Shirika la Global Alliance for Improved Nutrition (Gain), Archard Ngemela,amesema kupitia program ya  Yeffa  wanawasaidia vijana hao kuboresha kilimo na mifumo ya chakula.

Amesema Gain kwa kushirikiana na Agra na Mastercard Foundation, wanatekeleza program hiyo ya miaka minne inayotekelezwa katika mikoa 12 ambapo lengo ni kuchagiza juhudi za serikali kuboresha maisha ya mkulima kwa kuongeza thamani ya biashara ya mazao na fursa za ajira kwa vijana na wanawake.

“Gain tunashiriki aktika mradi huu upande wa lishe,tunaangalia usalama  wa chakula kuanzia uzalishaji hadi mwisho,teknolojia zinazotumika katika kuongeza urutubishaji wa vyakula iwe viwandani au mashambani,”amesema

“Tunawasaidia  vijana wajue taratibu,teknolojia zilizopo katika kuzalisha vyakula vyenye lishe lakini vinavyoendana na viwango ili wapate soko la mazao yao na kuongeza kipato,”

Mmoja wa wanufaika wa program hiyo,ambaye ni mkulima kijana, Jackline Robert amesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo hasa kuzingatia usalama wa chakula na kuwa wamejifunza umuhimu wa uongezaji virutubishi katika makundi manne  ambayo  hutumika katika milo ambayo ni unga wa mahindi,unga wa ngano,mafuta ya kupikia na chumvi.

“Kwa sababu baadhi ya magonjwa ambayo siyo ya kuambukiza yanasababishwa na kukosekana kwa viutubisho katika vyakula vyetu,tumejifunza njia za usindikaji vyakula na kuongeza virutubisho kwa kuzingatia usalama,”amesema

Awali akifungua mafunzo hayo,Mwakilishi kutoka Ofisi ya Ofisa Elimu Mkoa wa Arusha,Mwalimu Tumsifu Mushi,amesema mafunzo hayo yatachochea ajira kwa vijana katika sekta ya kilimo,kuongeza ufanisi wa kuyafikia masoko,kuongeza uzalishaji na utekelezaji wa miongozo mbalimbali.

“Sote tunatambua dunia inakabiliwa na changamoto ya usalama wa chakula na mamilioni ya watu duniani kote wanakabiliwa na njaa,utapiamlo na mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri uzalishaji wa chakula ,”amesema

“Hii ni hasara kubwa hivyo tukishirikiana tunaweza kujenga mifumo ya chakula ambayo inahakikisha  usalama wa chakula kwa wote,inalinda mazingira na inachangia maendeleo endelevu,”ameongeza