Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana 5 ,000 kupewa nyenzo kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwenye sekta ya kilimo

Mratibu wa tamasha la Wakulima Festival 2025, Fadhili Alison akitoa taarifa ya ujio wa tamasha hilo kwa waandishi wa habari hawapo pichani  litakalifanyika kuanzia Aprili 25 mpaka 30 mwaka huu. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Maonyesho ya tamasha la Wakulima Festival 2025  yameandalia na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na programu ya  Dynamic Agricature litakalo kutanisha Taasisi zaidi ya 100 nchini.

Mbeya. Vijana 5,100 kutoka vijiji 51, Tarafa ya Isangati Wilaya ya Mbeya,  kujengewa uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwenye sekta ya kilimo  kwa  kugeukia  matumizi ya teknolojia za kisasa  kupitia Tamasha la Wakulima Festival 2025.

Tamasha hilo limeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,  kwa kushirikiana na Dynamic Agricature Programu linalotarajiwa kuanza Aprili 25 mpaka 30  ,mwaka huu  likiwa la kwanza mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 16,2025 Mratibu wa tamasha hilo ,Fadhili Alison amesema lengo ni kuwajengea uwezo vijana kutambua fursa za kilimo katika  kuchangia pato na  uchumi  wa nchi.

Fadhili ambaye pia ni Meneja programu, amesema maonyesho hayo yamelenga kuzifikia  Kata 9 , vijijini 51, vyenye wananchi 90, 785 ,Wilaya ya Mbeya sawa na kaya 23,969 kwa takwimu ya  sensa ya watu na makazi 2020.

Ametaja sababu ya kufanyika katika maeneo ya vijijini ni kutoa fursa kwa wakulima kupitia shamba darasa,huku  taasisi zaidi ya 100 za masuala ya  kilimo zitashiriki .

Amesema wanatarajia kupokea wageni mbalimbali wa kitaifa ndani ya siku sita za maonyesho na  kubainisha tayari maandalizi yanaendelea vizuri.

Ofisa Masoko  kutoka Kampuni ya Mbolea Tanzania(TFC),Mkoa wa Mbeya, Laurent Joseph,amesema kupitia kongamano hilo  wamelenga kuwafikia wakulima wa chini kuhakikisha wanafikiwa na pembejeo za kilimo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya serikali.

"Miaka ya sasa kilimo ni sayansi  tutaendelea kutoa elimu kwa wakulima kutumia teknolojia za  upimaji wa afya ya udongo ili kufikia malengo ya serikali ya awamu ya sita katika uwekezaji wa sekta ya kilimo,"amesema.

Amesema kama taasisi ya serikali watashiriki kikamilifu ,lengo ni kuwafanya wakulima kuzalisha kizalendo na kuwa na matumizi sahihi ya mbolea .

Mkulima ,Witness Kamwela amesema programu hiyo italeta suruhisho la kudumu na kuondoa changamoto katika sekta ya kilimo hususani kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

"Miaka ya sasa kuna shida kubwa katika uzalishaji ,lakini ujio wa tamasha la Wakulima Festival 2025 ,uwenda likawa chachu ya kugeukia teknolojia za kisasa katika uzalishaji,"amesema.