Vigogo sita wakutwa na hatia baraza la maadili, yumo hakimu

Baadhi ya wajumbe na watu waliohudhuria katika kikao cha Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma.
Muktasari:
- Baraza la Maadili kwa Viongozi wa Umma limesikiliza malalamiko ya vigogo sita kati ya tisa waliofikishwa kwenye baraza hilo na kuwatia hatiani.
Dodoma. Vigogo sita, akiwemo Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Puge Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora, Cleophas Mziray, wametiwa hatiani na Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kutowasilisha tamko la rasilimali na madeni kwa Kamishna wa Maadili, jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Wengine waliofikishwa mbele ya baraza hilo na kujikuta wakiingia kitanzini ni madiwani wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, Mwandei Mohamed (Mtimbwani) na Mussa Buhero (Mayomboni), pamoja na Msajili wa Hati Msaidizi Mkoa wa Tanga, Mwajuma Kihiyo.
Vigogo hao wamefikishwa mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Rose Teemba, leo Alhamisi Machi 27, 2025, na kusomewa mashtaka yao. Wote walikiri kutowasilisha tamko hilo.
Katika mashtaka hayo, upande wa Sektarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, umeongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Emma Geleni, ambaye amesaidiana na Hassan Mayunga, Lidya Mwakibete, na Hilary Hassan.

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Puge mkoani Tabora, Cleophas Mziray
Walalamikiwa walitiwa hatiani kwa nyakati tofauti kwa kutowasilisha matamko yao ya rasilimali na madeni, kama kinavyoelekeza kifungu cha 9(1B) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na hivyo kukiuka kifungu cha 16(A) cha sheria hiyo.
Akisoma mashtaka mbele ya Diwani Mwandei, Wakili Emma alieleza kuwa mlalamikiwa huyo aliingia katika uongozi kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 na mwaka huo aliwasilisha tamko la rasilimali na madeni, lakini mwaka 2021 hakuwasilisha.
Alipoulizwa na mwenyekiti wa baraza hilo, Jaji Mstaafu Teemba, diwani huyo alikiri na kutiwa hatiani kwa kukiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Adhabu iliyomwendea pia Diwani Buhero, baada ya kuonekana makosa yao yakishabihiana.
Kuhusu Hakimu Mziray, Wakili Mayunga amesema kiongozi huyo ameongoza tangu mwaka 2010, lakini ameshindwa kutimiza matakwa ya sheria ya kuwasilisha tamko la rasilimali na madeni kwa miaka mitatu mfululizo (2022 hadi 2023).
Alipoulizwa na mwenyekiti wa baraza hilo, Jaji staafu Teemba alikiri kutowasilisha tamko hilo, hivyo baraza kumtia hatiani.
Msajili wa Hati Msaidizi wa Mkoa wa Tanga, Mwajuma Kihiyo, ametiwa hatiani kwa kutokuwasilisha tamko la raslimali na madeni kwa miaka miwili (2022 na 2023), wakati alishika nafasi hiyo tangu 2020.
Tofauti na washitakiwa wengine, Mwajuma ambaye muda wote alikuwa amejiinamia katika ukumbi wa baraza, hali iliyoonyesha hofu ya kujutia kosa lake na kutopenda kuonyesha uso wake kwa watu waliokuwa ndani ya ukumbi.
Kwenye malalamiko yanayomuhusu Columba, baraza limemtia hatiani baada ya kukiri kutowasilisha tamko lake kama anavyopaswa kwa mujibu wa sheria kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo (2022 na 2023).
Hata hivyo, Columba amesema kumbukumbu zinamuonyesha kuwa alijaza fomu za tamko hilo kwa mwaka 2022, lakini hana hati ya kuthibitisha.
Kwa upande wa mwaka 2023 alichelewa kujaza fomu hizo, lakini alipoulizwa zaidi ya mara tatu alikiri kutojaza, ndipo Jaji mstaafu Teemba alihitimisha kusema, “Umekiri hukujaza fomu kwa wakati uliotakiwa, baraza litaendelea na utaratibu unaotakiwa, unaweza kwenda.”
Kwa upande wa mlalamikiwa Mhina, Wakili Lidya amedai kuwa mwaka 2022 na 2023 hakuwasilisha tamko lake la rasilimali na mali kama sheria inavyotaka. Akijitetea, Mhina amesema anakubaliana na maelezo hayo na kuwa kosa hilo limetokana na changamoto katika njia ya utumaji wa fomu hizo zilizojitokeza hapo awali. Lakini, baada ya kuanza kutumika kwa utaratibu wa kujaza kwa njia ya mtandao, kosa hilo halitajitokeza tena.
Baada ya kumaliza kusikiliza shauri hilo, Jaji mstaafu Teemba ameahirisha baraza hilo hadi Machi 28, 2025, ili kumalizia vigogo waliobakia, ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, Sakina Mohamed, Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Jacob Rombo, na Diwani wa Kolero mkoani Morogoro, Eligius Mbena.

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora, Idefonce Columba
Tofauti na washitakiwa wengine Mwajuma ambaye muda wote alikuwa amejiinamia katika ukumbi huo wa baraza,hali iliyoonyesha hofu ya kujutia kosa lake na kutopenda kuonyesha uso wake kwa watu waliokuwa ndani ya ukumbi.
Kwenye malalamiko yanayomuhusu Columba Baraza limemtia hatiani baada ya kukiri kutowasilisha tamko lake kama anavyopaswa kwa mujibu wa sheria kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo ambayo ni 2022 na 2023.
Hata hivyo, Columba amesema kumbukumbu zinamuonyesha kuwa alijaza fomu za tamko hilo kwa mwaka 2022 lakini hana hati ya kuthibitisha na kwa upande wa mwaka 2023 alichelewa kujaza fomu hizo lakini alipoulizwa zaidi ya mara tatu alikiri kutojaza ndipo Jaji Mstaafu Teemba alihitimisha kuwa, “Umekiri mwenyewe hukujaza fomu kwa wakati uliotakiwa, baraza litaendelea na utaratibu unaotakiwa, unaweza kwenda.”
Kwa upande wa mlalamikiwa Mhina, Wakili Lidya amedai kuwa Mhina katika mwaka 2022 na 2023 hakuwasilisha tamko lake la raslimali na mali kama Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inavyotaka.
Akijitetea Mhina amesema anakubaliana na maelezo hayo na kuwa kosa hilo limetokana na changamoto katika njia ya utumaji wa fomu hizo zilizojitokeza hapo awali lakini baada ya kuanza kutumika kwa utaratibu wa kujaza kwa njia ya mtandao kosa hilo halitajitokeza tena.
Baada ya kumaliza kusikiliza shauri hilo, Jaji Mstaafu Teemba ameahirisha baraza hilo hadi Machi 28,2025,wakapomalizia vigogo waliobakia ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita Sakina Mohamed, Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Jacob Rombo na Diwani wa Kata ya Kolero mkoani Morogoro Eligius Mbena.